Home Uncategorized POLISI TANZANIA: TUNAZITAKA POINTI TATU ZA MWADUI

POLISI TANZANIA: TUNAZITAKA POINTI TATU ZA MWADUI


MARCEL Kaheza mshambuliaji wa Polisi Tanzania amesema kuwa leo watakuwa na kazi kubwa ya kuzisaka pointi tatu mbele ya Mwadui FC kwenye mchezo utakaochezwa Uwanja wa Kambarage.

Kaheza amekuwa kwenye ubora wake msimu huu chini ya Malale Hamsini ambaye ni Kocha Mkuu wa Polisi Tanzania amehusika kwenye mabao tisa kati ya 27 waliyofunga Polisi Tanzania akifunga mabao matano na pasi nne za mabao.
Akizungumza na Saleh Jembe, Kaheza amesema kuwa wamekuwa wakipewa mbinu nyingi zinazowafanya wawe bora jambo analoamini litawapa matokeo chanya kwa wapinzani wao.
“Kocha amekuwa akitupa mbinu nyingi na nzuri ambazo zinaeleweka na tunazifuata tukiwa uwanjani kutafuta matokeo tuna amini kwamba tutapata matokeo kwenye mechi zetu zote tunazocheza tunahitaji pointi tatu,” amesema Kaheza.
SOMA NA HII  YANGA YAFICHUA SIRI YA USHINDI KWA ALLIANCE