Home Habari za michezo KISA KAGOMA …AHMED ALLY “ATUPA JIWE JEUSI KWENYE SHIMO LA KIZA”….

KISA KAGOMA …AHMED ALLY “ATUPA JIWE JEUSI KWENYE SHIMO LA KIZA”….

Habari za simba-Kagoma

MENEJA wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Simba, Ahmed Ally ametupa dongo kwa wapinzani wao kuwa wataendelea kuteseka baada ya kiungo wao, Yusuph Kagoma amerejea uwanjani.

Kagoma alikosa mechi na Dodoma Jiji kutokana na jeraha alilopata katika mchezo wa Azam FC , Jumatano Oktoba 2, amerejea uwanjani kufanya mazoezi na wachezaji wenzake kujiandaa na mchezo wa kesho (leo) dhidi ya Coastal Union.

Ahmed Ally amesema kuwa baada ya kukaa nje kwa muda wa siku saba Kagoma yupo fiti , kucheza mechi ya kesho (leo) ni mipango ya benchi la ufundi linaloongozwa na Kocha Fadlu Davids.

Amesema kuumia wa nyota huyo katika mchezo na Azam FC alilazimika kukaa nje kwa ajili ya kutibu majeraha yake na hakusimamishwa na Kamati ya hadhi na haki za wachezaji.

“Mashine ya kuchanganyia zenge imerudi kazini , mtaweka wapi sura zenu, wale mliosema kiungo wetu amesimamishwa kupisha kesi ucharwa. Mungu akipenda Ijumaa (leo) tutaendelea kupata raha za Kagoma,” amesema Ahmed.

SOMA NA HII  ZILIPENDWA:...ADHABU YA CAF KWA MATOLA YAIVURUGA SIMBA...TFF WAJIFUNGIA KUJADILI...