Habari za Simba Leo

MO DEWJI KUONGOZA MKUTANO WA SIMBA LEO

Abubakar October 6, 2024 11:25 am

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Simba, MO Dewji leo atakuwepo kuuongoza mkutano mkuu wa mwaka wa Simba Sports Club utakaofanyika kwenye ukumbi wa Kimataifa wa JNICC.

Murtaza Mangungu Mwenyekiti wa Simba na Makamu Mwenyekiti wa Bodi pia atakuwepo.

Leo hii Simba Sports Club inafanya mkutano wake wa kila mwaka kujadili mambo mbalimbali yanayoihusu klabu yao.

Ikumbukwe kwamba Mo Dewji amerudi rasmu Simba kwa msimu huu, na kuvunja makundi yote yaliyokuwepo katika klabu hiyo.

Pia Mo Dewji amefanya usajili mkubwa sana kwa msimu huu ikiwemo kuvunja mikataba ya wachezaji ambao, viwango vyao havikuwa vizuri.

UTAMU WA KUBASHIRI NA MERIDIANBET NI ODDS KUBWA …. HATIMAYE MO DEWJI ATAMBULISHA MCHORO WA UWANJA WA SIMBA