Habari za Simba Leo

YALIYOJIRI KWENYE MKUTANO WA SIMBA LEO…MO DEWJI AOMBA MCHAKATO WA MABADILIKO UKAMILIKE

Abubakar October 6, 2024 1:15 pm

MOHAMED DEWJI Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Simba na Rais wa Heshima wa klabu hiyo amesema kuwa, ili mambo ya maboresho ya Simba yatimie inatakiwa mchakati wa mabadiliko ukamilike.

Mo Dewji amesema kwamba mchakati wa mabadiliko wa Simba upo katika hatua za mwisho kukamilika.

“Ili kufanikisha yote haya tunasubiri mchakato wa mabadiliko ya Simba kukamilika. Tuko katika hatua za mwisho. Ujenzi wa miundombinu hii unakuja na gharama kubwa, ni ngumu kuanza huu ujenzi bila mfumo kubadilika.”

“Tukishirikiana tunaweza kujenga Simba inayoweza kushindana ubingwa wa Klabu Bingwa Afrika, malengo haya sio ndoto, bali ni lengo linaloweza kufikiwa. Pamoja tunaijenga Simba ya kesho.”

“Huu ni wakati wa kuchukua hatua kwa nguvu zaidi.

“Tukimaliza mchakato wa mabadiliko Simba itakuwa tayari kusimama imara na kujitegemea. Kwa heshima kubwa naomba tuache fitna, tuache fitna tuwe kitu kimoja.

Tusigawanyike.” Amesema Mo Dewji.

HATIMAYE MO DEWJI ATAMBULISHA MCHORO WA UWANJA WA SIMBA MANGUNGU NA MO DEWJI WAPIGIANA MAKOFI.