HABARI ZA SIMBA NA YANGA
Habari za michezo

CAF WALIVYOIPELEKA ‘DABI’ YA SIMBA NA YANGA ALGERIA…SHOW NZIMA ITAKUWA HIVI…

admin October 12, 2024 4:46 pm

Kwa mara ya kwanza, timu za Simba na Yanga zitakuwa nchini Algeria kwa wakati mmoja (ndani ya wiki moja) kwenye mechi za michuano ya CAF, kila timu ikiwa na kibarua chake.

Wiki hiyo ni ile yenye tarehe 6-8 mwezi Desemba mwaka huu, ambapo Simba itakwenda kucheza mchezo wa raundi ya pili hatua ya makundi Kombe la Shirikisho dhidi ya CS Costantine ambayo maskani yake ni katika mji wa Costantine…. Wakati Yanga ikiwa Algiers kucheza dhidi ya MC Alger, mchezo wa hatua hiyohiyo kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika…

Mechi hizi huenda zikapishana kwa siku moja hadi mbili lakini pia huenda zikepigwa katika miji tofauti ambayo ni Costantine na Algiers.

Je, Simba na Yanga ‘kuivamia’ Algeria kwa wakati mmoja kusaka alama tatu za CAF, unapata picha gani????

Ratiba ya Simba iko hivi:-

28/11/2024: Simba vs Bravos.
08/12/2024: Costantine vs Simba.
15/12/2024: Simba vs Sfaxien.
05/01/2025: Sfaxien vs Simba.
12/01/2025: Bravos vs Simba.
19/01/2025: Simba vs Costantine.

Ratiba kamili ya yanga iko hivi:-
26/11/2024: Yanga vs Al Hilal.
06/12/2024: MC Alger vs Yanga
13/12/2024: TP Mazembe vs Yanga
03/01/2025: Yanga vs TP Mazembe
10/01/2025: Al Hilal vs Yanga
17/01/2025: Yanga vs MC Alger.

YANGA NA HESABU ZA ROBO FAINALI ZIKO HIVI. BAADA YA MAISHA YAKE YA SIMBA KUPITA…..CHAMA AFICHUA HILI LA CAF NA YANGA….

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

One response to “CAF WALIVYOIPELEKA ‘DABI’ YA SIMBA NA YANGA ALGERIA…SHOW NZIMA ITAKUWA HIVI…”

  1. […] Mlango wa Simba na Yanga Ally Salim Katolo na mwenzake AbdulTwalib Mshery wanategemewa sana na taifa, lakini nafasi zao za […]