Home Habari za michezo MSHERY NA ALLY SALIM WANATEGEMEWA NA TAIFA.

MSHERY NA ALLY SALIM WANATEGEMEWA NA TAIFA.

Habari za Simba SC

WALINDA Mlango wa Simba na Yanga Ally Salim Katolo na mwenzake AbdulTwalib Mshery wanategemewa sana na taifa, lakini nafasi zao za kucheza kwenye vilabu vyao ni finyu.

Hayo yamesemwa na Mchambuzi wa michezo nchini kupitia kituo cha redio cha Crown Fm, Magunga.

“Golikipa Abuutwalib Mshery ( Yanga Sc ) na Ally Salim (Simba sc ) wanategemewa zaidi kwenye mahitaji ya ndani ya timu ya Taifa lakini hawachezi mechi ya kutosha kwenye vilabu vyao na inawezekana wanashindwa kuondoka kutokana na ukata wa fedha uliopo ndani ya vilabu vingine ukilinganisha klabu walizopo kwa sasa”

“Mshery kwasasa Yanga Sc hapati namba sana kutokana na uwepo wa golikipa namba moja Diarra anafanya vizuri zaidi ila pia Ali Salim atumiki sana baada ya uwepo wa Moussa Camara”

SOMA NA HII  MAYELE:- KUNA KIPINDI NILILAZIMIKA KUKATAA KUCHEZA YANGA ....