Kwa mara ya kwanza, timu za Simba na Yanga zitakuwa nchini Algeria kwa wakati mmoja (ndani ya wiki moja) kwenye mechi za michuano ya CAF, kila timu ikiwa na kibarua chake.
Wiki hiyo ni ile yenye tarehe 6-8 mwezi Desemba mwaka huu, ambapo Simba itakwenda kucheza mchezo wa raundi ya pili hatua ya makundi Kombe la Shirikisho dhidi ya CS Costantine ambayo maskani yake ni katika mji wa Costantine….
Wakati Yanga ikiwa Algiers kucheza dhidi ya MC Alger, mchezo wa hatua hiyohiyo kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika…
Mechi hizi huenda zikapishana kwa siku moja hadi mbili lakini pia huenda zikapigwa katika miji tofauti ambayo ni
Costantine na Algiers.
Je, Simba na Yanga ‘kuivamia’ Algeria kwa wakati mmoja kusaka alama tatu za CAF, unapata picha gani????
[…] ameongea hayo baada ya Yanga kupangwa Kundi A la Ligi ya Mabingwa Afrika, ikiwa na timu za TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasi […]