Home Habari za michezo HUU HAPA MKAKATI ULIVYO WA AFCON KUPIGWA MARA MBILI NCHI ZA CECAFA…

HUU HAPA MKAKATI ULIVYO WA AFCON KUPIGWA MARA MBILI NCHI ZA CECAFA…

Habari za Michezo leo

Ethiopia imetangaza nia ya kuwasilisha maombi ya kuwa mwenyeji wa mashindano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) mwaka 2029.

Rais wa Ethiopia Taye Atske Selassie ameyasema hayo katika Mkutano Mkuu wa 46 wa Shirikisho la Soka Afrika (CAF), unaoendelea katika mji mkuu wa Ethiopia Addis Ababa.

β€œTumewekeza kwenye maendeleo na miundombinu ya michezo kama mkitupa nafasi tutakuwa wenyeji wa mashindano ya AFCON 2029 ninachukua nafasi hii kuiomba CAF kuiruhusu Ethiopia kuwa mwenyeji wa Mashindano ya AFCON 2029” amesema Rais huyo.

Mkutano huo ulioanza jana umehudhuriwa na Rais wa Shirikisho la Soka Duniani (FIFA) Giovanni Infantino, maafisa kutoka Mashirikisho ya soka ya nchi wanachama wa CAF, Mashirikisho ya soka ya kanda, na wadau wengine maarufu wa mchezo wa soka duniani kote.

Kama Ethiopia itafanikiwa kushinda tenda ya kuwa mwenyeji wa mashindano hayo kwa mara nyingine baada ya mwaka 1976 ukanda wa CECAFA utakuwa mwenyeji wa mashindano hayo kwa mara ya pili mfululizo baada ya AFCON ya mwaka 2027 itakayofanyika Tanzania,Kenya na Uganda.

SOMA NA HII  KUELEKEA MECHI ZA KUFUZU β€˜AFCON 2023’...TAIFA STARS HAWATAKI MZAHA AISEE...WAAMUA KUTUMIA MBINU ZA SIMBA....