Home Habari za michezo DIARRA AFICHUA YANGA WALIVYOMPA “SHAVU” NCHINI KWAO MALI…’WANANIOMBA SANA JEZI’….

DIARRA AFICHUA YANGA WALIVYOMPA “SHAVU” NCHINI KWAO MALI…’WANANIOMBA SANA JEZI’….

HABARI ZA YANGA-DIARRA

KIPA wa Yanga, Raia wa Mali, Djigui Diarra amesema ubora wa ligi ya Tanzania imempa nafasi ya kuitwa na kuaminika katika kikosi cha timu ya Taifa ya nchini humo.

Amesema Ligi ya Tanzania ni kubwa na bora sana, nzuri anafahamu kuwa kuna mechi zinatowa ushindani mkubwa mfano mchezo wa Simba na Yanga, Yanga na Azam FC, mechi ngumu sana na zinaonyesha taswira ya ubingwa.

Diarra ameweka wazi na kusema kuwa tangu amejiunga na Yanga wamekuwa wakimfatilia sana na hata anaporudi kucheza timu ya Taifa wanamuulizia kuhusu Yanga na kumuomba jezi.

“Watu wengi nchini Mali wanaijua na kuifatilia Yanga, nacheza ligi hii, ninapata nafasi ya kuitwa timu ya Taifa, ligi bora na kila ninavyosalia hapa nakuwa katika kiwango kizuri, naipenda sana Tanzania.

Wachezaji wenzangu wa timu ya Taifa, wengi wanaifahamu Yanga kuanzia mtaani wanafunzi mpaka mashabiki kwa kuwa wanafahamu nacheza hapa na wanaipenda hii timu,” amesema kipa huyo wa Yanga.

Kuhusu Ligi na mashindano ya Kimataifa, Diara amesema msimu huu wako vizuri na wanafanya maandalizi mazuri ya michuano ya Kimataifa, matarajio yake kufanya vizuri na kucheza fainali ya Afrika kwa sababu wana timu nzuri.

“Tuna wachezaji wazuri kama Stephane (Aziz ki), Pacome (Zouzoua), Kouassi (Attohoula Yao), Abutwalib (Mshery), Ibrahim (Bacca) kwa hiyo tuna kila sababu ya kufanya vizuri mpaka benchi la ufundi lipo vizuri.

Sote malego ya klabu ni kushinda ubingwa wa Ligi na Kimataifa, binafsi malengo yangu ni kushinda ligi na kufanya vizuri Ligi ya Mabingwa tutacheza fainali msimu huu Mungu akipenda nawaahidi tutacheza,” amesema Diarra amewapongeza mabeki wake kwa kumfanya anakuwa bora siku zote.

SOMA NA HII  SUALA LA MABADILIKO YANGA BADO KIDOGO KUKAMILIKA, FCC WATAJWA