Home Habari za michezo BAADA YA KUWAKANDA NAMUNGO JUZI….CHE MALENO AVUNJA UKIMYA SIMBA….

BAADA YA KUWAKANDA NAMUNGO JUZI….CHE MALENO AVUNJA UKIMYA SIMBA….

Habari za Simba leo

BEKI wa Simba, Che Maleno Fondoh amesema wanaweza kupata idadi kubwa ya mabao kwenye michezo ijayo wakiendelea kucheza kwa kasi waliyocheza mechi na Namungo FC.

Amesema ushindi ulioupata dhidi ya Namungo FC umeongeza morali na kuwapa hamasa ya kupambana zaidi katika michezo iliyopo mbele yao ikiwemo dhidi ya JKT Tanzania

Simba atakuwa mwenyeji kwenye mchezo ujao dhidi ya JKT Tanzania utakaochezwa kesho Jumanne Oktoba 29, uwanja wa KMC, Mwenge Dar es Salaam.

Che Malone amesema wakiendelea kucheza kwa kasi na kujitoa katika mchezo ujao dhidi ya JKT Tanzania watafunga idadi kubwa ya mabao.

β€œMchezo wetu na JKT Tanzania ni mgumu sana kwa sababu timu tuliocheza nao mara mbili mechi za kirafiki, tunajua vizuri tunatakiwa kucheza kwa kasi na kudhibiti safu ya ushambuliaji inayoongozwa na John (Bocco).

Ina wachezaji wengi ambao wametoka Simba wanaifahamu vizuri, tumerudia uwanja wa mazoezi kocha kutueleza tunaingia kwa mfumo gani kulingana na wapinzani wetu,” amesema Beki huyo.

Ameongeza kuwa wanahitaji kutafuta ushindi kufikia malengo yao ya kutwaa ubingwa wa ligi bado upo na anaimani kufanya vizuri zaidi kwenye michezo iliyopo mbele yao.

SOMA NA HII  KISA USHINDI DHIDI YA YANGA....WACHEZAJI IHEFU WAZIDI KUOGA MAMILIONI...MATAJIRI WAPAGAWA...