Home Habari za michezo KISA USAJILI WA MPANZU …KOCHA AS VITA ‘ATEMA CHECHE’ KWA SIMBA…

KISA USAJILI WA MPANZU …KOCHA AS VITA ‘ATEMA CHECHE’ KWA SIMBA…

Simba SC

Kaimu Kocha Mkuu wa AS Vita ya DR Congo, Raoul Shugu amesema Simba wamepata mtu kumsajili aliyekuwa mchezaji wa timu yake, Elie Mpanzu ambaye amejiunga na kikosi cha wekundu hao wa msimbazi kwa mkataba wa miaka miwili.

Kocha huyo amesema anafahamu uwezo wa Mpanzu kwani anaweza kucheza winga na namba 10 kulingana na matwaka ya kocha hivyo atawasaidia Simba kufikia malengo yao.

β€œMchezaji mzuri kabisa ana uwezo wa kufunga mabao mengi sana na atawasaidia, usimuone umbile lake dogo suala la mpira mguuni yuko vizuri,” amesema Shungu.

Ameongeza kuwa Simba wamepata mtu wa kusaidiana na waliopo ndani ya timu hiyo na kupata kile ambacho kinatarajiwa kwa mashabiki kuona timu hiyo inapata mataji.

Itakumbukwa kuwa Mpanzu amesajiliwa Simba kwa mkataba wa miaka miwili na ataanza kuwatumikia wekundu wa msimbazi kuanzia dirisha dogo la usajili.

Hata hivyo usajili wake umekuja kwa lengo la kuboresha kikosi cha timu hiyo ambacho kinaendelea kufanya vyema kwenye meci zaΒ  ligi ya NBC .

Hata hivyo inaelezwa kuwa Simba pia ipo mbioni kuongeza vyuma vingine vya maana kwa ajili ya michuano ya kimataifa, huku wakitazamia haswa kuongeza kwenye upande wa beki, na mshambulaiji mwingine hatari zaidi ya waliopo.

SOMA NA HII  HUYU HAPA MRITHI WA KAJUL NA BARBARA SIMBA...UWAYEZU FRANCOIS REGIS