Home Habari za Simba Leo HUYU HAPA MRITHI WA KAJUL NA BARBARA SIMBA…UWAYEZU FRANCOIS REGIS

HUYU HAPA MRITHI WA KAJUL NA BARBARA SIMBA…UWAYEZU FRANCOIS REGIS

Habari za Simba- Uwayezu Francois Regis

UONGOZI wa Simba umefikia makubaliano ya kumwajiri Uwayezu Francois Regis raia wa Rwanda kuwa Afisa Mtendaji Mkuu wa klabu hiyo, ili achukue nafasi ya Imani Kajula anayejiandaa kumaliza mkataba mwezi ujao.

Kajula ambaye ni mzoefu katika uongozi wa mpira, akiwamo kwenye Kamati ya maandalizi ya Michuano ya Afrika ya vijana chini ya umri wa miaka 17 yaliyofanyika nchini mwaka 2019 alijiunga na Simba kuzipa pengo la Barbara Gonzalez aliyejiondoa Januari mwaka jana baada ya awali kutangaza dhamira Desemba, 2022.

Chanzo cha kuaminika kutoka ndani ya Simba kimesema kuwa mazungumzo na Francois yamefika hatua nzuri kilichobaki ni kufikia muafaka wa kumalizana naye ili aweze kuipngoza Simba.

Francois, kwa sasa ni Makamu Mwenyekiti wa APR ya Rwanda na amewahi pia kuwa Katibu Mkuu wa Chama cha Soka cha Rwanda (FERWAFA).

“Kajula anakamilisha mkataba wake tu ndani ya Simba lakini makubaliano ya kumalizana endapo mkataba ukiisha yamefanyika na ndio maana uongozi umeamua kufanya mazungumzo na Francois ili kuchukua nafasi yake,” kilisema chanzo hicho.

Hii itakuwa ni mara ya pili kwa Simba kuwa na CEO kutoka nje ya nchi, kwani awali iliwahi kumuajiri, Senzo Mbatha kutoka Afrika Kusini ambaye baadaye alijiondoa na kutua Yanga kabla ya kurithiwa na Mzambia, Andre Mtine aliyetokea klabu ya TP Mazembe ya DR Congo.

Je ujio wa CEO huyo mpya utaleta tija kwa klabu ya Simba yenye malengo makubwa kwa soka la ndani na la Kimataifa, huku kukiwa na hitajio la kuongeza vyanzo vingi vya mapato.

Simba chini ya Imani Kajula ilifanikiwa kwa kiasi chake kuwavutia wadhamini na makupuni mbalimbali kuweka pesa zao ikiwemo kuanzisha Mtandao waMashabiki wa Simba Excutive Network SEN.

Pia Imani Kajula katika uongozi wake Simba imetwaa mataji ya Ngao ya Jamii mara moja, Kombe la Mapinduzi mara moja, Kombe la Muungano ambalo lilirejea tena msimu uliopita, huku kifanikiwa kutinga kwa mara nyingine hatua ya robo fainali ya Klabu Bingwa Afrika.

Lakini pia ndio kipindi ambacho Simba imemaliza katika nafasi ya 3 kwenye msimamo wa Ligi Kuu ya NBC baada ya miaka mingi kupita, na kuangukia katika Kombe la Shirikisho Afrika, kuhusu ubingwa wa Ligi Kuu lipo wazi tangu Kajula aingie madarakani Simba haijatwaa Kombe la Ligi kuu hata FA.

SOMA NA HII  DUCHU, CHILUNDA NJIA PANDA SIMBA....BENCHIKHA AWAKA HASIRA AKITAKA WAACHWE....