Home Habari za michezo DUCHU, CHILUNDA NJIA PANDA SIMBA….BENCHIKHA AWAKA HASIRA AKITAKA WAACHWE….

DUCHU, CHILUNDA NJIA PANDA SIMBA….BENCHIKHA AWAKA HASIRA AKITAKA WAACHWE….

Habari za Simba leo

Kocha Mkuu wa Simba SC Abdelhah Benchikha amewaambia wachezaji wake kuwa kila mchezaji atampa nafasi ya kucheza katika Kombe la Mapinduzi na yule atakayeshindwa kumuonyesha ubora wake, basi panga litampitia katika usajili huu wa dirisha dogo.

Kauli hiyo imekuja baada ya kucheza mchezo wao wa kwanza wa Kombe la Mapinduzi na kupata ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya JKU katika Uwanja wa New Amaan Complex, Zanzibar.

Simba SC imepanga kukifanyia maboresho kikosi chao katika usajili huu wa dirisha, kwa kuingiza maingizo mapya na kuwaacha wengine ambao wameshindwa kupambana kusaka namba kikosi cha kwanza.

Taarifa zinaeleza kuwa, Benchikha tayari ametangaza hataki mchezaji wa kukaa benchi, badala yake anataka yule wa kucheza katika kikosi cha kwanza.

Mtoa taarifa huyo amesema kuwa, alianza hilo katika mchezo wa kwanza wa Kombe la Mapinduzi kwa kuwaanzisha wachezaji waliokosa nafasi ya kucheza katika ligi ya michuano ya kimataifa mabeki Jimmyson Mwanuke, David Kameta ‘Duchu’ na mshambuliaji Idd Chilunda ambao kocha hajafurahishwa na viwango vyao.

Amesema kuwa anaendelea kutoa nafasi ya kucheza kwa wachezaji hao wa benchi, na kabla usajili haujafungwa ripoti yake ya usajili kwa wachezaji wa kuwaacha na kuwatoa kwa mkopo itakamilika kwa kuwaleta wengine wapya watakaongeza chachu ya ushindani.

“Kocha amekasilishwa na baadhi ya wachezaji wake ambao amewakuta na kushindwa kuonyesha viwango bora kwa wale ambao hawakupata nafasi ya kucheza katika ligi na michuano ya kimataifa.

“Kocha ametangaza kuwa hataki kuwa na wachezaji wa benchi katika timu yake, anataka kuona kila mchezaji akipambania namba na kuingia katika kikosi cha kwanza.

Na anatumia Kombe la Mapinduzi kuwaangalia wachezaji ambao hawakupata nafasi nyingi ya kucheza kwa kumshawishi kuonyesha kiwango bora, kwa wale watakaoshindwa, basi kocha atawaacha na wengine kutolewa kwa mkopo kwa ajili ya kulinda vipaji vyao.

“Chilunda, Duchu na Mwanuke kocha aliwapa nafasi ya kucheza katika mchezo dhidi ya JKU, lakini wameshindwa kuonyesha kiwango bora, bado ataendelea kuwapa wengine,” amesema mtoa taarifa huyo.

Kocha huyo mara baada ya mchezo dhidi ya JKU, alionekana kukasirishwa na viwango vya baadhi ya wachezaji na kutamka kuwa:”Sifurahishwi na baadhi ya wachezaji wakiwemo baadhi ya mabeki ambao walianza katika kipindi cha kwanza.

“Sitakuwa tayari kumvumilia mchezaji ambaye anashindwa kuonyesha ushindani wa namba katika timu, hivyo nitatoa mapendekezo kwa viongozi kuachana na baadhi ya wachezaji walioshindwa kunishawishi uwanjani.”

Jana Simba pia ilijitupa uwanjani kwenye muendelezo wa Kombe la Mapinduzi ambapo walipata ushindi wa magoli 2-0 dhidi ya Singida Fountain Gate .

Magoli ya Simba katika mchezo huo uliokuwa wa aina yake yalifungwa na Andrew Onana, pamoja na Luis Miquissone.

SOMA NA HII  KOCHA GEITA GOLD:- WALETENI HAO YANGA...TUNAAPA KULIPA KISASI