Home Habari za Simba Leo MO DEWJI AFANYA KIKAO KINGINE SIMBA…SASA AKUTANA NA WANACHAMA WA SEN

MO DEWJI AFANYA KIKAO KINGINE SIMBA…SASA AKUTANA NA WANACHAMA WA SEN

HABARI ZA SIMBA- MO DEWJI

Rais na Mwenyekiti wa Bodi ya Simba, Mohammed MO Dewji amekutana na kufanya mazungumzo na Simba Executive Network (SEN).

SEN ni mtandao wa mashabiki wa Simba ambao huchangia ada ya 1,500,000 kwa mwaka kwa ajili ya miradi maalumu ya miundombinu ya klabu. Wanachama wa SEN hupata faida nyingi kama bima za maisha, tiketi za mechi na faida nyingine nyingi.

Kikao hicho kilihudhuriwa na Viongozi wa SEN akiwapo Mwenyekiti Abdulrazak Badru, Makamu wake Farouk Baghoza, Katibu Dkt. George Ruhago, Katibu Msaidizi Richard Mwalibwa na wanachama wa SEN. Menejimenti ya Simba iliongozwa na Afisa Mtendaji Mkuu, Imani Kajula.

Lengo la kikao hicho lilikuwa ni kufanya tathimini ya jinsi ya kuimarisha Simba mpya, na kuweka mipango mikakati imara ya baadae kuhusu klabu hiyo.

Itakumbukwa kwamba Kikosi cha Simba kipo nchini Misri katika mji wa Ismailia kujiandaa na msimu mpya wa 2024/25.

Kambi ya timu hiyo inaendelea kupamba moto baada ya kikosi kamili cha Msimbazi kutimia huku kukiwa na taarifa za Willy Onana zikieleza kwaba Uongozi wa Mnyama umempigia simu na kumwambia aripoti kambini haraka.

Tayari Onana ameanza taratibu za kurudi Tanzania huku akitafuta VISA yake mpya ya kusafiria hadi Misri, Hapo awali Simba walikuwa wanaitaka saini ya Winga wa AS Vita Elie Mpanzu lakini kuna taarifa za kwamba Rais wa timu hiyo ametaka dau la dola 150000 sawa na zaidi ya Tsh milioni 600, kwa mchezaji aliyebakiza mkataba wa miezi 4 pekee.

Kurejea kwa Willy Onana Simba huenda ikawa ndio dili la kuinasa saini ya Mpanzu kushindikana na mnyama huenda wameweka mahesabu ya kumsubiri awe mchezaji huru kisha wamchukue.

SOMA NA HII  RASMI...CAF WAIPITISHA SIMBA KUSHIRIKI AFRICAN SUPER LEAGUE...WATAPEWA BILI 5.8...TFF NAO WATAAMBULIA BIL 2...