Home Habari za Simba Leo KAMBI YA SIMBA MISRI YAMPA MZUKA AUGUSTINE OKEJEPHA, MWENYEWE AFUNGUKA

KAMBI YA SIMBA MISRI YAMPA MZUKA AUGUSTINE OKEJEPHA, MWENYEWE AFUNGUKA

Habari za Simba- Augustine Okejepha

KIUNGO mkabaji mpya wa Simba, Mnigeria Augustine Okejepha amesema amefurahishwa na maandalizi ya timu hiyo yanayoendelea kambini, Ismailia Misri, huku akiweka wazi kila mchezaji kwa sasa anaonyesha anataka kukipambania kikosi hicho msimu ujao.

Nyota huyo aliyejiunga na Simba akitokea Rivers United ya Nigeria, alisema licha ya ugeni wake ndani ya timu hiyo na kutozoeana na wachezaji wenzake ila amefurahia namna walivyompokea jambo linalompa imani mbeleni.

“Nafurahia mazingira ya huku, na jinsi mapokezi yangu yalivyokuwa, maandalizi ni mazuri na nimeyapenda” Alisema Augustine Okejepha.

Simba wakati wanamtambulisha mchezaji huyo walisema kwamba wanaamini Okejepha ataenda kutibu ugonjwa wa muda mrefu kwenye eneo la Kiungo wa Ulinzi, akisaidiana na Fabrice NGOMA na Mzamiru Yassin pia Yusuph Kagoma.

“Ni rasmi tumekamilisha usajili wa kiungo mkabaji raia wa Nigeria kutoka Rivers kwa mkataba wa miaka mitatu. Okejepha ni mchezaji kijana mwenye miaka 20 aliyetunukiwa kipaji kikubwa katika idara ya kiungo wa ulinzi.

“Katika miaka kadhaa sasa tumekuwa tukihitaji kupata mchezaji ambaye ataipa uimara safu yetu ya ulinzi na Okajepha anatarajia kuwa suluhisho.

“Okejepha ndiye mchezaji bora wa Ligi Kuu ya nchini Nigeria (MVP) kwa msimu 2023/2024,” ilisema taarifa hiyo.

“Ujio wa Okejepha unalifanya eneo la kiungo cha ukabaji ndani ya Simba msimu ujao atakuwepo yeye, Mzamiru Yassin, Fabrice Ngoma, Sadio Kanoute na Yusuph Kagoma ambaye taarifa zilizopo ni kwamba muda wowote atatambulishwa kikosini hapo.”

Augustine Okejepha ulikuwa ni usajili wa sita kutambulishwa ndani ya Simba kuelekea msimu ujao baada ya Valentino Mashaka, Abdulrazack Mohamed Hamza, Jean Charles Ahoua, Steven Mukwala na Joshua Mutale.

Pia Simba imetangaza kuwaongezea mikataba Kibu Denis, Israel Mwenda na Mzamiru Yassin huku ikiachana na Kennedy Juma, Shaban Chilunda, Luis Miquissone, Saido Ntibazonkiza, John Bocco na Henock Inonga aliyeuzwa kwenda FAR Rabat ya Morocco.

Clatous Chama naye ameondoka Simba baada ya mkataba wake kumalizika akiitumikia timu hiyo kwa takribani misimu sita na sasa ametua Yanga.

SOMA NA HII  KWISHA KAZIIII....MANGUNGU ARIDHIA KUWA MWENYEKITI 'BUBU' SIMBA....KATIBA YAPITISHWA....