Home Habari za Simba Leo WAZIR JUNIOR KUHUSU KUIFUNGA SIMBA…AMTAJA BOCCO, WAWA NA YONDANI WA...

WAZIR JUNIOR KUHUSU KUIFUNGA SIMBA…AMTAJA BOCCO, WAWA NA YONDANI WA YANGA

HABARI ZA SIMBA NA YANGA- WAZIRI JUNIOR

Kila binadamu huwa na ndoto zake lakini sio kazi rahisi kuifikia ndoto unayoiota kila siku, kutana na Kijana wa Kitanga “The Kingi of CCM Kirumba” Wazir Junior jinsi ambavyo aliwahi kupata uchungu uliomfanya aweke nadhiri kwa Mungu.

Wazir Junior anasema kila mchezaji ana historia ya alipotokea hadi kufikia hatua ya kujulikana mbele ya jamii, akiamini yapo ya kujifunza kutokana na hatua za mafanikio yao.

“Mfano mzuri wengi wanapenda wanachokifanya mastaa wa nje kama Cristiano Ronaldo, Lionel Messi, Kylian Mbappe na wengine wengi, ila nyuma yao kuna hatua walizopitia, zipo za kuumiza na kufurahisha, lakini mwisho wa yote kilichowafanya vipaji vyao vionekane kwa ukubwa, hawakuruhusu kukata tamaa.

“Kuna nyakati nimewahi kupitia, hadi nikawa nawaza kwamba labda kuna sehemu nimekosea, ila kuna siku niliamua kukaa chini na kufanya uamuzi wa kuhakikisha sikubali kipaji changu kipotee.”

KUHUSU KUIFUNGA SIMBA.

Wazir Junior haifungi Simba kwa bahati mbaya, bali ni dhamira aliyoiweka Septemba 2013 akiwa anatoka katika geti la Uwanja wa Kinesi uliopo Shekilango jijini Dar es Salaam.

Maneno yanaumba kama anavyosimulia Junior kwamba: “Nilitoka kufanya majaribio katika kikosi cha Simba B. Kuna maneno niliambiwa ambayo yaliniumiza sana moyo. Kabla ya kulivuka geti la Uwanja wa Kinesi nilisema Mungu nifungulie milango ya kupata timu ili nikija kukutana na Simba niwe naifunga.

“Siwezi kusema ni maneno gani na niliambiwa na nani. Ila kwa mara ya kwanza kucheza Ligi Kuu ilikuwa 2015 nikiwa na Toto Africans, bao pekee nililoifunga Simba liliiathiri ikakosa ubingwa na taji likaenda kwa Yanga.

“Nikiwa na Mbao FC niliifunga Simba mabao mawili, KMC mabao mawili hivyo nimeifunga jumla ya mabao matano ukijumlisha na la Toto Africans. Nitaendelea kuifunga hadi Mungu atakapoamua nisiifunge. Pia mashabiki wajue Yanga nimeifunga kama ninavyoweza kuzifunga timu nyingine.”

ALIFELI WAPI YANGA

Yanga ilimsajili Wazir Junior akitokea Mbao FC na timu ilikuwa chini ya kocha Cedrick Kaze, ambapo awali alishindwa kupata nafasi, lakini baada ya ujio wa Nasreddine Nabi akawa anacheza baadhi ya mechi na kukaa benchi.

“Nilisajiliwa Yanga wakati kocha ni Kaze nilicheza mechi moja. Baada ya kuja Nabi nikawa napewa dakika chache za kucheza na pia nilikuwa nakaa benchi, hivyo jibu sahihi kilichonifelisha ni kukosa nafasi ya kucheza,” anasema.

Anafichua pia alichoambiwa na Nabi kwamba alikuwa anapenda ushambuliaji wake wa kutokea nyuma ya mabeki.

Anakiri kuona mashabiki mitandaoni wakimsema akienda timu kubwa anashindwa kuonyesha uwezo wake, lakini anataka wafahamu jambo moja, kuna ugumu kwa wazawa thamani zao kufanana na wageni ndani ya klabu hizo.

“Kitu kigumu kwa mchezaji ni kutokucheza, hali hiyo inaweza ikamtoa mchezoni, lakini ninawashauri wanaobahatika kusajiliwa katika klabu hizo, waongeze juhudi ya mazoezi na kuhakikisha wanawashawishi makocha ili wapangwe na kuonyesha uwezo wao,” anasema.

SOMA NA HII  SIKU KADHAA TOKA ASEPE MSIMBAZI ...MHILU AVUNJA UKIMYA...AFUNGUKA MAZITO KUHUSU SIMBA NA MO DEWJ...