Home Taifa Stars NGORONGORO HEROES WAPANGWA KUNDI LA KIFO AFCON

NGORONGORO HEROES WAPANGWA KUNDI LA KIFO AFCON


HATIMAYE droo ya makundi ya fainali za mataifa ya Afrika kwa vijana wenye umri chini ya miaka 20 (Afcon U-20) imechezeshwa leo Jumatatu Januari 25 kwenye hoteli ya Hilton mjini Yaounde Cameroon na kila timu kujua ipo timu gani.

Droo hiyo ilihusisha timu za taifa za vijana (U-20) kutoka nchi 12 zilizofuzu kucheza michuano hiyo ambazo ni Mauritania, Burkina Faso, Cameroon, Jamhuri ya Afrika ya kati, Gambia, Ghana, Morocco, Mozambique, Namibia, Tanzania, Tunisia na Uganda.

Katika makundi hayo timu ya Tanzania ‘Ngorongoro Heroes’ imepangwa kwenye kundi linaoloonekana kuwa la kifo kwani lina timu vigogo kwenye historia ya Soka la Afrika.

Ngorongoro wamepangwa na Gambia, Ghana na Morocco kwenye kundi  C.

Makundi mengine ni A lenye timu za Cameroon, Uganda, Mozambique na wenyeji Mauritania, pia kundi jingine ni B lenye timu za Burkina Faso, Tunisia, Namibia na Jamhuri ya Afrika ya kati.

Ngorongoro Heroes ilifuzu kucheza michuano hiyo mikubwa barani Afrika baada ya kuweza kufika fainali ya kombe la mataifa ya Afrika Mashariki na Kati (CECAFA) yaliyomalizika mwezi Desemba mwaka jana kwenye viwanja vya shule ya Black Rhino iliyopo Arusha nchini Tanzania.

Katika mashindano hayo Uganda waliibuka mabingwa baada ya kuifunga Tanzania bao 4-1 kwenye mchezo wa fainali za michuano hiyo iliyohusisha jumla ya timu tisa za  Burundi, Djibouti, Sudan, Kenya, Somalia, Sudan Kusini, Tanzania, Uganda na Ethiopia, huku Eritrea na Rwanda wakijiondoa.

Tayari kikosi cha Ngorongoro Heroes kipo kambini Jijini Arusha tangu Januari 13 kikijiandaa kwaajili ya michuano hiyo ambayo inatarajiwa kuanza mwezi Februari nchini Maurtania.

SOMA NA HII  FT: TANZANIA 0-3 DR CONGO...A-Z JINSI STARS 'WALIVYONYANYASWA' UWANJANI..MATUMAINI BADO...