Home Habari za Simba Leo SIMBA YAMALIZANA NA AUGUSTINE OKEJEPHA…AANZA SAFARI RASMI.

SIMBA YAMALIZANA NA AUGUSTINE OKEJEPHA…AANZA SAFARI RASMI.

Habari za Simba

KIUNGO mkabaji wa Rivers United, Mnigeria Augustine Okejepha ameeleza dili lake la kujiunga na Simba, huku akisisitiza shauku yake kubwa ni kucheza soka la Tanzania licha ya kuwa na ofa kutoka klabu zingine nje ya nchi hiyo.

Kwa mujibu wa Mwanaspoti Okejepha amesema ni kweli wako katika mazungumzo na viongozi wa Simba, lakini bado hajasaini mkataba wa kuichezea msimu ujao.

“Ni kweli tuko katika mazungumzo, ila siwezi kusema moja kwa moja kwa sasa kwa sababu bado hatujafikia uamuzi wa mwisho. Napenda sana kucheza Tanzania kwani ni ligi yenye ushindani ambayo imekuwa ikivutia nyota wengi kujiunga nayo,” amesema.

Mnigeria huyo mwenye umri wa miaka 20, amesema mbali na Simba inayomtaka, lakini kuna ofa zilizo mezani kwa uongozi wa timu anayoichezea ikiwemo ya FC Ural Yekaterinburg kutoka Urusi inayoshiki Ligi Daraja la Kwanza.

“Wapo wachezaji wengi kutoka Nigeria ambao walipita au wapo hadi sasa hivi katika soka la Tanzania kama Nelson Okwa (aliwahi kucheza Simba sasa Plateu United ya Nigeria), Victor Akpan (kakipiga Coastal Union na Simba sasa ni mchezaji huru), Benjamin Tanimu na Morice Chukwu (Singida Black Stars), hivyo nami napenda kuona nikiwa sehemu kama hiyo,” amesema.

Okejepha aliyewahi kuchezea Kano Pillars aliyojiunga nayo akitokea Warri Wolves FC zote za Nigeria, inaelezwa kwamba tayari ameanzasafari ya kuja Dar kumalizana na Simba.

Mnigeria huyo atachukua nafasi ya Babacar Sarr ambaye inasemekana atapewa Thank You, baada ya kushindwa kufanya vizuri akiwa amedumu Msimbazi kwa nusu msimu, alisajili dirisha dogo.

Tayari Simba imeshatangaza kuachana na wachezaji na nahodha wa timu hiyo, John Bocco, Shaaban Idd Chilunda, Saido Ntibazonkiza ‘Saido’ na Kennedy Juma huku ikimtambulisha beki wa kati, Lameck Lawi kutoka Coastal Union.

Afisa Habari wa Simba, Ahmed Ally ALizungumzia juu ya usajili huo alikaririwa akisema wakati huu ni wa usajili na kila mchezaji anatajwa kujiunga na timu hiyo na kwamba hawawezi kujibu kila kitu kinachoendelea.

“Hili ni dirisha la usajili na mengi yanazungumzwa. Nikisema nizungumzie kila mchezaji anayetajwa kutua Simba nitachoka. Naomba hili tuliache kwanza kwani muda wa kutambulisha wachezaji tuliowasajili ukifika tutafanya hivyo,” alisema Ahmed.

SOMA NA HII  PHIRI MAMBO MAGUMU SIMBA, MKATA UMEME KUTOKA TOGO HUYU HAPA MSIMBAZI