Home Habari za Simba Leo INONGA AIPATIA SIMBA MIL 500…WAARABU WAMALIZA KILA KITU

INONGA AIPATIA SIMBA MIL 500…WAARABU WAMALIZA KILA KITU

Habari za Simba leo

ALIYEKUWA Beki wa Simba Henock Inonga amejiunga na FAR Rabat ya Morocco baada ya timu hiyo kufuata saini yake.

FAR Rabat imezungumza na Simba ikitaka huduma ya beki huyo Mkongomani ambapo zimejadiliana kufanya biashara na dau la zaidi ya Sh500 milioni linatajwa kufikiwa.

Inonga ambaye ana mkataba wa mwaka mmoja kuendelea kuitumikia Simba uamuzi wa kumuuza umekuja baada ya mabosi kuona dau walilowekewa linawashawishi huku kiwango cha chini uwanjani alichoonyesha msimu uliopita na majeraha yaliyomkabili ni sababu zingine zinazotajwa kuuzwa kwake.

Taarifa kutoka ndani ya Simba zinasema kwamba, bodi ya klabu hiyo imeridhia kumuuza Inonga kwenda FAR Rabat kwa dau hilo.

“Simba tunachosubiri ni kuingizwa tu kwa fedha hizo kwani tayari tumeshakubaliana kila kitu. Bora aende huko tuwe na timu mpya kwa msimu ujao,” amesema bosi mmoja kutoka ndani ya bodi ya klabu hiyo.

“Inonga ni beki mzuri kama ambavyo nilikwambia huko nyuma kwamba huu msimu uliopita umetuchafua sana, tukakosa raha. Ndio maana tulimtaka kama ana ofa ailete tumpe nafasi ya kuondoka kwa amani.”

Wakati Inonga akitajwa kuondoka Msimbazi tayari Simba imeshaanza msako wa haraka wa kutafuta beki mpya wa kati atakayechukua nafasi yake ikiendelea na mazungumzo na mabeki wa maana ikianza na Lameck Lawi wa Coastal Union.

Simba pia inaangalia uwezekano wa kuwa na beki kutoka nje ya Tanzania ambpao miongoni mwa wanaotajwa ni Anthony Tra Bi Tra anayecheza ASEC Mimosas.

SOMA NA HII  YALIYOJIRI KWENYE MKUTANO WA SIMBA LEO…MO DEWJI AOMBA MCHAKATO WA MABADILIKO UKAMILIKE