Home Habari za michezo KWA USAJILI WA MASTAA HAWA SIMBA…MSIMU UJAO WAKIKOSA UBINGWA HAWAPATI TENA YANI…

KWA USAJILI WA MASTAA HAWA SIMBA…MSIMU UJAO WAKIKOSA UBINGWA HAWAPATI TENA YANI…

Habari za Simba leo

SAFARI HII Simba hawatanii, katika usajili ndiyo imeanza hivyo kwa kushusha mastaa watatu huku wawili kati yao ni kutoka nje na mmoja wa hapa wa hapa ndani.

Msimu ujao wa 2024/25 utakuwa mtamu kuliko unavyofikiri maana mastaa wanaoshushwa na Simba wanajua boli kweli kweli.

Msemaji wa Simba Ahmed Ally mewaweka wazi mikakati yao ikiwemo suala la usajili wa nyota wapya na kuweka wazi mastaa wanaohusishwa kusajiliwa.

mastaa hao wenye uchu wa mataji ni kiungo mkabaji Augustine Okejepha kutoka Rivers United ya Nigeria, Elie Mpanzu kutika AS Vita ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo, Sergie Pokou wa Asec Mimosas ya Ivory Coast wakiungana na mtoto wa nyumbani hapa hapa Yusuph Kagoma akitokea Singida Fountain Gate.

Ahmed ameongeza kwamba mastaa hao walioonyesha viwango vikubwa walipokuwa wakizitumikia timu zao za awali na watachukua nafasi za wachezaji ambao hawakuwa na wakati mzuri ndani ya Simba.

Wachezaji wanaotajwa kupokea mkono wa kwa heri kwa kupewa ‘Thank You’ ni pamoja na Pa Omary Jobe, John Bocco, Bakar Sarr, Said Kanoute, Saido Ntibazonkiza na Kennedy. Wengine ni Aishi Manula, David Kameta, Inonga Baka, Khamis Abdalah, Ahmed  Teru na Luis Miquissone.

Ahmed amesema usajili wa Elie Mpanzu, amesema kuwa muda ukifika watanaika jina lake na mastaa wote watakowasajili msimu huu.

“Ni mchezaji mzuri anavutia kucheza Simba, kumsajili au kutomsajili kwa hilo siwezi kusema kwa sasa ila  viongozi wa juu wanafanya mazungumzo na nyota huyo basi muda ukifika tutaweka wazi.

Suala la Kagoma tunaheshimu mkataba wake na Singida, tunaheshimu masuala ya mkataba wa mchezaji na timu yake, kiungo mzuri ana uwezo wa kukata umeme kwa ubora aliokuwa nao anauwezo wa kushika dimba Simba,” amesema Meneja huyo,

Hatma ya kiungo wao, Aubin Kramo amesema ametibiwa na daktari amejiridhisha baada ya kupata vipimo kuwa yupo tayari kurejea uwanjani na atakuwa sehemu ya wachezaji ambao wataenda nchini Misri kwa ajili ya Kambi, muda kwa kufurahia uwezo wake umekaribia.

“Kuhusu kutoa ‘thank you’, zoezi linaendelea, lilisimama kwa muda kwa sababu ya wachezaji ambao tunatarajia kuwaacha bado wana mikataba tunamalizana nao kwa kuwapa stahiki zao na tutakapowatema basi tuwe huru na kuepukana na kesi za kupelekana FIFA,” amesema Ahmed.

Amesema usajili mzuri unafanywa na ikiwemo kuvunja mkataba kwa mchezaji ambaye haonekani kuwa msaada ndani ya kikosi cha Simba kwa msimu ujao uongozi utalazimika kuvunja mkataba ili kupisha mwingine kusaidia timu kufikia malengo.

“Malengo yetu msimu ujao kufanya vizuri katika mashindano ya kombe la shirikisho ikiwemo kucheza nusu au fainali, kufikia huku lazima tufanya usajili mkubwa kwa kuleta wachezaji wazuri watakaofika malengo yetu,” amesema Ahmed.

SOMA NA HII  KUMBE YANGA NAO HAWAJAMALIZA.... CHUMA HIKI HAPA JAGWANI