Home Habari za Simba Leo SIMBA YAPIGA PESA ZA WAARABU DILI LA INONGA.

SIMBA YAPIGA PESA ZA WAARABU DILI LA INONGA.

Habari za Simba leo

UONGOZI wa Simba SC umetangaza kuachana na mchezaji wao Kitasa Henock Inonga ambaye atajiunga na AS Far Rabat ya nchini Morocco.

Simbe jioni ya Juni 24 wamethibitisha juu ya biashara ya mchezaji huyo kukamilika na kila upande umeridhika.

Taarifa ya Simba imeweka wazi kwamba, Makubaliano ya kumuuza mchezaji huyo ambaye ni Raia wa DR Congo yamekamilika na hatokuwa sehemu ya kikosi chao kwa msiku ujao.

“Klabu yetu imefikia makubaliano ya kumuuza mlinzi wa kati Henock Baka kwenda AS Far Rabat”

“Baada ya kuitumikia timu yetu kwa misimu mitatu, Henock Inonga Baka hatokuwa sehemu ya kikosi cha msimu ujao”

Haya yote yanajiri baada ya kuwepo tetesi kwa kipindi kirefu kuwa mchezaji huyo anahitajika na aliyekuwa kocha wa Yanga Nasradinne Nabi, ambaye alikuwa anafundisha AS Far ya huko Morocco.

Na inaelezwa kwamba Inonga alishafikia makubaliano na waarabu hao ambapo alisaini mkataba nao Juni 14 mwaka huu alipokuwa na timu ya taifa ya DR Congo kwenye kambi.

Inonga alikuwa amebakiza msimu mmoja ili awe huru, kwani mkataba wake na Simba ulikuwa unaisha Mei 2025, hivyo kwa maana hiyo ni kwamba Simba wamepiga hela kwenye dili na ndicho walichokuwa wanakitaka.

Awali Soka la Bongo tuliripotu juu ya taarifa za usajili wa mchezaji huyu, kwani kila kitu kijulikana mapema, na hata leo Juni 24 tulifahamu fika juu ya taarifa za Henock Inonga kuondoka Simba.

SOMA NA HII  HAO SIMBA HUKO SUPER LEAGUE, HAPA AL AHLY PALE MAMELODI SIO POA