Home Habari za Simba Leo MAKOSA MAWILI YA KIBU DENIS NA TIMU YAKE MPYA…SIMBA YAWEKA SHARTI HILI.

MAKOSA MAWILI YA KIBU DENIS NA TIMU YAKE MPYA…SIMBA YAWEKA SHARTI HILI.

Habari za Simba SC

BAADA ya SOLD OUT ya Simba Day Klabu hiyo sasa imetoa sharti gumu kwa mchezaji wake Kibu Denis na Kristiansund BK inayomhitaji ili imruhusu mshambuliaji huyo kujiunga na timu hiyo inayoshiriki Ligi Kuu ya Norway.

Sharti hilo ni kuitaka Kristiansund BK kulipa kiasi cha Dola 1 milioni (Sh 2.7 bilioni) ili kumnunua moja kwa moja mshambuliaji huyo vinginevyo haitokuwa tayari kumuachia kwa dau la fedha chini ya hilo.

Mmoja wa viongozi wa Simba ameiambia Mwananchi kuwa wamefikia uamuzi huo ili kutoa fundisho kwa wachezaji na klabu za soka kuheshimu mikataba kama miongozo ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Duniani (Fifa) inavyofafanua.

“Kuna makosa matatu makubwa ambayo yamefanyika katika suala hilo la Kibu (Denis) ambayo Simba tukisema tusichukue hatua hatuwezi kusaidia soka hasa katika suala la kuheshimu mikataba kwa wachezaji na timu. Kosa la kwanza ni mchezaji kuidanganya klabu na kutorika akijua kabisa ana mkataba tena wa muda mrefu ambao ametoka kuusaini.

“Kosa la pili limefanywa na hiyo timu ya Norway la kufanya mazungumzo kinyemela na mchezaji wa timu nyingine ambaye bado ana mkataba huku ikiwa kinyume na kanuni za Fifa na kosa la tatu ni mchezaji kuharibu taswira ya klabu kwa kusema uongo kuwa inafahamu7 sababu ya kutokuwepo kambini huku ikiwa kinyume chake,” amesema kiongozi huyo.

Kwa mujibu wa kiongozi huyo, Simba imetoa sharti kwa klabu hiyo ya Norway kuvunja mkataba kwa dau la Dola 1 milioni na kinyume na hapo itaishtaki.

“Tumeona na kusikia upande wa mchezaji unajaribu kutuomba na kutushawishi tumuuze kwenda Norway lakini kwa dau wanalotaka wao jambo ambalo sio sawa na linazidi kumuweka huyo mchezaji matatizoni. Msimamo wa klabu haujabadilika ambao ni kuitaka hiyo timu imnunue moja kwa moja mchezaji kwa dau la Dola 1 milioni na sio kufanya majaribio ya mwezi mzima kama wanavyotaka.

“Ikishindikana tutaishtaki hiyo timu kwa Fifa kwa kosa la kumtorosha mchezaji wetu na uthibitisho wote tunao ambao ni barua ya kuomba radhi ambayo Kristiansund wametuandikia na pia ya ofa waliyoileta mezani lakini pia uthibitisho wa mchezaji mwenyewe,” amefafanua kiongozi huyo.

Meneja wa Kibu Denis, Carlos Sylivester alinukuliwa akisema kuwa upande wao watakaa na Simba ili kutafuta suluhisho la shauri hilo lililojitokeza.

“Kibu anapaswa kufahamu, hakuna namna anaweza kuikwepa Simba kwani ana mkataba nao kama kuna jambo lolote ni vizuri kukaa mezani azungumze na viongozi wake kusudi jambo hili lifikie kikomo,” alinukuliwa Sylivester.

SOMA NA HII  UNAAMBIWA HUYO AYOUB WA SIMBA BADO HAJAANZA BALAA LAKE