Home Habari za Simba Leo JULIO ATIA NENO SAKATA LA CHAMA…ATOA MIFANO YA MIAKA YA NYUMA

JULIO ATIA NENO SAKATA LA CHAMA…ATOA MIFANO YA MIAKA YA NYUMA

STAA YANGA:- PACOME ANATUMIA NGUVU NYINGI...CHAMA ANATUMIA AKILI NYINGI...ANAMCHAMBUA HADI KIPA

Jamhuri Kiwelu Julio ameingilia kati sakata la mchezaji wa Simba Clatous Chama ambaye inasemekana amekataa kuongeza mkataba mpya kwa madai ya kuongezewa stahiki zake.

Chama anahusishwa zaidi na Yanga kama ataachwa na miamba hiyo ya mtaa wa Msimbazi, jambo hili limemnyenyua aliyewahi kuwa mchezaji wa timu ya Simba Julio na kutoa maoni yake juu ya hatma ya Chama.

Akizungumza na kituo cha Habari cha Redio One Jijini Dar Es Salaam Julio alisema kwamba, Chama ni mchezaji wetu tunamuheshimu isipokuwa tabia zake.

“Nampongeza na kumsifia sana Magori, ni kiongozi shupavu ambaye yakitokea mambo kama haya hawezi kupaka paka rangi, kasema yeye kama anataka aondoke, aende kwa sababu wachezaji wenye uwezo kama yeye na kumzidi wapo wengi”

“Viongozi wasimtetee Chama kama anataka kuondoka aonde, Simba ina uwezo wa kununua wachezaji wazuri vile vile, kwa sababu ni binadamu leo akifa, au kavunjika mguu Simba haichezaji? Itaendelea kucheza, Mimu Julio nilipita Simba leo sipo, na Kama Chama hataki kuongeza mkataba mpya anataka kwenda timu nyingine wamuache aende, atakuja Chama mwingine” Alisema Jamhuri Kiwelu Julio.

Wiki nzima hii sasa kumekuwa na habari nyingi kuhusu mchezaji huyo kuondoka Simba, na hadi jana jioni kwa Taarifa tulizozipata ni kwamba Bado Chama hajasaini Yanga wala Simba, japokuwa Mohammed Dewji “MO” amemuita kwenye kikao siku ya Alhamis 27, ili kujadili mustakabalu wa mchezaji huyo kwa undani wake.

CHAMA anataka kulipwa Tsh Milioni 50, huku akitaja dau lake la usajili kuwa ni zaidi ya Tsh Mil 700.

Uongozi wa Simba kwa sasa upo tayari kwa lolote kuhusu Chama, akikubali kuongeza mkataba mpya kwa masharti waliyompatia sawa, au akikataa kuongeza mkataba basi wapo tayari kumuacha akatafute Changamoto mpya kwingine, japo anapewa nafasi kubwa zaidi ya kujiunga na Yanga.

SOMA NA HII  YANGA KUTAMBULISHA KIFAA KIPYA...AUCHO AWAPA RAMANI YOTE