Home Habari za Simba Leo HENOCK INONGA AAGA SIMBA…UJUMBE HUU AMEANDKA NA KUFUTA

HENOCK INONGA AAGA SIMBA…UJUMBE HUU AMEANDKA NA KUFUTA

Habari za Simba

BEKI wa Simba SC Henock Baka Inonga amewaaga mashabiki wa Klabu hiyo kwa kumpokea na kumfanya adumu katika klabu hiyo misimu mitatu.

Inonga ametumia mitandao yake ya kijamii ikiwemo Instagram kuwaaga mashabiki wa klabu ya Simba.

Beki huyo baada ya kuwa nje kwa kipindi kirefu baada ya kupata majeraha kwenye mechi ya Dabi, ambapo Simba ilipoteza mchezo huo kwa mabao 2-1, huku bao la kusawazisha la Simba likifungwa na Fred Michaele.

Inonga mapema hii leo ameandika ujumbe huu kuwaaga mashabiki wa timu hiyo;

“Asante sana kwa familia nzima (Simba) Nimekuja kusema asante kwa yote mliyonifanyia nadhani leo nilitaka kusema Kwaherini”

“Asante familia, utabaki moyoni mwangu kila wakati” Aliandika Henock Inonga.

Baada ya kuandika ujumbe huu, mchezaji huyo aliufuta mara moja wakati huo tayari Soka LA Bongo tulikuwa tumeshaunasa.

Simba imetangaza kutoa taarifa mpya majira ya Saa 1 za Usiku, kwahiyo huenda itakuwa ni taarifa ya kumuaga mchezaji wao Henock Inonga baada ya kudumu kwa misimu zaidi ya miwili, huku akiwa ni moja ya wachezaji pendwa kwa mashabiki wa Simba.

Inaelezwa kwamba mchezaji huyo alikuwa anahitajika na Far Rabat ya nchini Morocco, lakini upepo umeanza kubadilika na kusemekana amepata timu moja ya Ufaransa.

Kwahiyo hadi sasa anapewa nafasi kubwa ya kuondoka Simba msimu kuliko kubaki.

SOMA NA HII  MCHEZAJI WA ZAMANI SIMBA...AISHITAKI TIMU YAKE FIFA