Home Habari za Simba Leo BAADA YA MUTALE SIMBA YAHAMIA KWA KIUNGO WA RIVERS UTD

BAADA YA MUTALE SIMBA YAHAMIA KWA KIUNGO WA RIVERS UTD

Habari za Simba

BAADA ya kudaiwa kumalizana na Joshua Mutale kutoka Zambia, mabosi wa Simba umeanza kumfuatilia kiungo mkabaji wa Rivers United, Augustine Okejepha ili atue kuiboresha timu hiyo msimu ujao.

Kiungo huyo (20), inadaiwa anaonwa ni chaguo sahihi Simba kwa ajili ya msimu ujao, japo timu mbalimbali zimeonyesha kuvutiwa naye ikiwemo, FC Ural ya Urusi inayoshiki Ligi Daraja la Kwanza.

Simba kupitia kamati ya usajili mpya, iliyo chini ya magwiji na wataalam wa kazi hizo Magori, Swedi Nkwabi, Kassim Dewji na Mulamu Mughambi tayari imeanza kufanya kazi za kimafia kwenye usajili wa wachezaji wengi wa kigeni.

Magori na wenzake wanasifika sana kwenye inshu za usajili na kupitia uwekezaji wa mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi, Simba mpya imeanza kusukwa na tayari sajili kadhaa za wachezaji wengi zikiwa zimekamilika, kinachosubiriwa tu ni kuanza kutambulishwa rasmi.

Zambia ni sehemu mooja wapo yenye vipaji vingi vya soka, ikumbukwe kuwa Chama alitoka huko, Moses Phiri, Rally Bwalya, ni mooja ya sajili za maana zilizowahi kucheza Simba na wengine bado wapo Simba.

Chama bado haijulikani itakuaje, lakini Mosses Phiri alitolewa kwa mkopo kwenda nchini kwao Zambia Zesco United.

MO Dewji  anahitaji sajili mpya za Mnyama  Simba, ziwe na vijana wadogo wenye uchu wa mafanikio na wenye nguvu ya upambanaji.

SOMA NA HII  HIZI HAPA SABABU ZA MSINGI MGUNDA KURUDISHWA SIMBA...."BAJETI YA MISHAHARA MIL 600"...