Home Habari za Simba Leo MGUNDA AFUNGUKA MAZITO…MASHABIKI KAENI KWA KUTULIA

MGUNDA AFUNGUKA MAZITO…MASHABIKI KAENI KWA KUTULIA

Habari za Simba

BAADA ya Jeshi zima la Simba kutua salama Ethiopia, Kocha Mkuu wa Simba Queens, Juma Mgunda, amesema wachezaji wake wanajua kilichowapeleka nchini humo na wanafahamu vyema matarajio ya Watanzania.

Simba Queens iko Ethiopia kwa ajili ya kushiriki mashindano ya Ligi ya Mabingwa wa Afrika Mashariki na Kati kwa Wanawake (CECAFA), yanayotarajiwa kufanyika kuanzia kesho hadi Agosti 31, mwaka huu.

Mgunda alisema wachezaji wote wako katika hali nzuri na wanaahidi watapambana kuhakikisha wanatwaa ubingwa wa michuano hiyo.

“Wandele (wasichana) wanajua kilichowafanya waje Ethiopia, licha ya kuwa na jukumu la klabu, lakini wanajukumu la kitaifa, wako vizuri na wako tayari,” alisema Mgunda.

Aliongeza kila mechi kwao itakuwa muhimu na hawatawadharau wapinzani wao kuanzia mechi ya kwanza watakaocheza Jumapili dhidi ya FAD kutoka Djibouti.

Simba ambayo imepangwa katika Kundi B itashuka tena dimbani Agosti 20, mwaka huu kuvaana na Kawempe Muslim FC kutoka Uganda na itamaliza mechi za hatua ya makundi dhidi ya mabingwa wa Burundi, PVP Buyenzi siku mbili baadaye.

Timu mbili zitakazomaliza katika nafasi mbili za juu zitatinga hatua ya nusu fainali na fainali ya mashindano hayo zitafanyika Agosti 21, mwaka huu.

SOMA NA HII  BALEKE AMFUKUZISHA KAZI KOCHA IHEFU...NI BAADA YA KUFANYIWA UKATILI HUU MKUBWA