Home Habari za Simba Leo MTACHAGUA LAKRED AANZE AU FABRICE EBOGO…SIMBA INAFANYA UMAFIA

MTACHAGUA LAKRED AANZE AU FABRICE EBOGO…SIMBA INAFANYA UMAFIA

habari za simba

Simba ipo kwenye mazungumzo ya kumpata mlinda mlango wa Cameroon, Joseph Fabrice Ondoa Ebogo ili kuboresha kikosi hicho.

Kipa huyo anayeichezea Nimes Olympique ya Ufaransa, anatajwa kama mbadala wa Ayoub Lakred ikiwa Simba itashindwa kumbakisha licha ya kuelezwa mazungumzo yameanza chini ya Mwekezaji na Rais wa Heshima, Mohammed Dewji ‘MO’.

Simba kupitia kamati ya usajili mpya, iliyo chini ya magwiji na wataalam wa kazi hizo Magori, Swedi Nkwabi, Kassim Dewji na Mulamu Mughambi tayari imeanza kufanya kazi za kimafia kwenye usajili wa wachezaji wengi wa kigeni.

Magori na wenzake wanasifika sana kwenye inshu za usajili na kupitia uwekezaji wa mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi, Simba mpya imeanza kusukwa na tayari sajili kadhaa za wachezaji wengi zikiwa zimekamilika, kinachosubiriwa tu ni kuanza kutambulishwa rasmi.

Che Malone Fondoh, Willy Essomba Onana ni baadhi ya wachezaji waliotoka nchi ya Cameroon, hivyo ujio wa kipa huyo kama kila kitu kitaenda sawa huenda klabu ya Simba ikawa na nyota watatu wa nchi mmoja.

Simba wanaendelea kujiimarisha kila upande hivyo kwa sasa kila kitu kinafanyika kimya kimya, huku baadhi ya watu wakijua Simba haina maelewano kumbe mabosi wa timu hiyo wanaandaa silaha nzito za kivita.

Baadhi ya wachezaji wameshasajili na kila  kitu kipo tayari,  kinachosubiriwa ni utambulisho wao.

SOMA NA HII  KWA UNDANI HAWA HAPA WAPINZANI WA SIMBA CAFCC.