Home Azam FC BAADA YA KUSHUSHA VIFAA VYA MAANA…AZAM FC KUFUNGA USAJILI NA KIFAA HIKI...

BAADA YA KUSHUSHA VIFAA VYA MAANA…AZAM FC KUFUNGA USAJILI NA KIFAA HIKI CHA HATARI KUTOKA IVORY COAST…


MABOSI wa Azam FC wamesema usajili wa kumnasa kiungo mkabaji kutoka Ivory Coast, Claude Singone kwa ajili ya kusaidia timu hiyo kufanya vizuri katika mechi za Ligi Kuu Tanzania Bara na mashindano ya kimataifa ya Kombe la Shirikisho Afrika watakayoshiriki utakuwa ni wa mwisho kuelekea msimu mpya.

Taarifa zilizopatikana jijini zinasema Singone alionekana akiwa na mmoja wa watendaji wa juu wa klabu hiyo kwa ajili ya kukamilisha usajili wake.

Ofisa Habari wa Azam FC, Thabit Zakaria ‘Zakazakazi’ , alisema baada ya kumtambulisha, James Akaminko kwa  kumpa mkataba wa miaka miwili, wako katika mchakato wa kumalizana na nyota mwingine wa kimataifa ambaye hakutaja jina lake.

Zaka alisema wanaendelea kufanya maboresho katika kikosi chao kwa kufuata mapendekezo yaliyotolewa na benchi la ufundi kwa kuzingatia nafasi zote.

“Ujio wa Akaminko utaimarisha zaidi kikosi cha timu yetu kulingana na uwezo wake wa kucheza nafasi nyingi, na tunatarajia kushusha kifaa kingine, tuko katika hatua ya mwisho kumalizana na beki wa kati wa kimataifa, huyu atafunga usajili wetu,” alisema Zaka.

Aliongeza baada ya kukamilisha usajili wa beki huyo timu itaingia kambini keshokutwa na Julai 22, mwaka huu wataelekea Misri kwa ajili ya kuweka kambi ya siku 20 ili kujiandaa na msimu mpya.

“Maandalizi ya safari yetu kuelekea Misri yamekamilika, tunatarajia wachezaji wetu wataimarika na kurejea nchini wakiwa na kasi na tayari kwa ajili ya kupambana, timu zote zimefanya usajili mzuri, hivyo nasi lazima tukajiwinde,” Zaka alisema.

Hadi sasa Azam FC imemamilisha usajili wa wachezaji watano wa kigeni ambao ni golikipa, Ali Ahamada ambaye ni raia wa Comoro, Isah Ndala, Tape Edinho, Kipre Junior, Akaminko na wachezaji wazawa ni pamoja na Nathaniel Chilambo, Cleophance Mkandala na Abdul Suleiman ‘Sopu’.

Azam FC ilimaliza Ligi Kuu Tanzania Bara msimu uliopita katika nafasi ya tatu nyuma ya mabingwa Yanga na Simba, zote za jijini huku Geita Gold FC ikishika nafasi ya nne na kupata tiketi ya kushiriki michuano ya kimataifa ya Kombe la Shirikisho Afrika.

SOMA NA HII  HIVI NDIVYO BAO 5 ZA YANGA ZINAVYOITESA SIMBA HADI LEO