Home Habari za michezo JAMBO LA SIMBA LATIKI MISRI…’MAVITUZ’ YA KOCHA MPYA SIO POA…MASTAA WANYOOSHWAAA…

JAMBO LA SIMBA LATIKI MISRI…’MAVITUZ’ YA KOCHA MPYA SIO POA…MASTAA WANYOOSHWAAA…


Washindi wa pili ndani ya Ligi Kuu Tanzania Bara, Simba tayari wameanza mazoezi nchini Misri ikiwa ni maandalizi kwa ajili ya msimu mpya wa 2022/23.

Simba chini ya Kocha Mkuu, Zoran Maki ilifanikiwa kuwasili nchini Misri salama baada ya kusepa Bongo Julai 14,2022 mchana.

Kwa mujibu wa Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano ndani ya Simba, Ahmed Ally ameweka wazi kwamba kila kitu kinakwenda sawa na wachezaji wanafurahia mazingira waliyopo.

“Tumefika salama Misri na wachezaji wameanza mazoezi kwa ajili ya msimu mpya chini ya kocha Maki ambaye anajua namna ya kuweza kuwapa mbinu wachezaji na tunaamini kwa muda ambao tutakuwa hapa kuna namna tutakuwa imara,”

Baadhi ya wachezaji ambao wapo nchini Misiri ni pamoja na Meddie Kagere, John Bocco,Chris Mugalu,Beno Kakolanya,Ally Salim,Gadiel Michael,Pape Sakho na Clatous Chama.

SOMA NA HII  SAA KADHAA TOKA ATEULIWE UKOCHA MKUU SIMBA... COASTAL UNION WAIBUKA NA HILI KUHUSU MGUNDA...