Home Habari za michezo HAPA NDIPO TUTAJUA MBIVU NA MBICHI SIMBA vs POWER DYNAMO

HAPA NDIPO TUTAJUA MBIVU NA MBICHI SIMBA vs POWER DYNAMO

Uwanja wa michezo wa Levy Mwanawasa ni Uwanja wa michezo uliopo katika mji wa Ndola nchini Zambia, uwanja huu hutumika sana kwa ajili ya mchezo wa mpira wa miguu ukiwa na uwezo wa kuchukua mashabiki 49,800. Serikali ya China ilitangaza kujenga uwanja huu mnamo mwaka 2010.mchezo wa kwanza wa kimataifa ulichezwa katika uwanja huu mnamo tarehe 9 Juni 2010 kati ya Zambia na Ghana na matokeo Zambiwa walishinda kwa bao 1-0.

Uwanja huu ulipewa jina la raisi wa tatu wa Zambia, aliefariki mwaka 2008.Levy Mwanawasa. Uwanja huu ndio utatumika katika Mchezo kati ya Power Dynamos Vs Simba hapo keshokutwa Jumamosi Septemba 16.

Uwanja huu ukiachana na timu ya taifa kuutumia pia hutumiwa na timu za Zesco United FC,Power Dynamo na Forest Rangers FC. Uzuri wa Uwanja huu Chama na Moses Phiri wanaufahamu vyema sana….Kila la Kheri Mnyama.

SOMA NA HII  SIMBA WABADILI GIA ANGANI KISA MPIRA HUU