Home Habari za michezo ALIYMBEBA MAYELE ATAKIWA HUKU

ALIYMBEBA MAYELE ATAKIWA HUKU

Habari za Michezo

Kocha wa Klabu ya Pyramids ya Misri anayoichezea Fiston Mayele, Mreno Jaime Pacheco ameripotiwa kutakwa na klabu ya Marseille ya Ufaransa ambayo kwa sasa haina kocha mkuu baada ya kuachana na aliyekuwa kocha wao Mhispania Marcelino Garcia Toral ambaye alijiuzulu nafasi hiyo kwa sababu binafsi.

Jamie Pacheco alijiunga na Pyramids FC Januari 2023,na kuiwezesha timu hiyo kumaliza wapili kwenye ligi kuu ya Misri na kupata nafasi ya kushiriki michuano ya Klabu Bingwa Afrika.

Ripoti kutoka nyumbani kwa Jaime Pacheco nchini Ureno zinaeleza kuwa jina la kocha huyo limependekezwa kwa Rais wa Klabu ya Marseille Pablo Longoria ambaye anataraji kufanya maamuzi siku chache zijazo.

SOMA NA HII  MASHABIKI WAYDAD WAFUATA NYAYO ZA SIMBA WAMEKIWASHA HUKO HATARI