Home Habari za michezo BAADA YA KUWAZIBUA HOROYA KIBABE….MAJINA YA MASTAA HAWA WA SIMBA YATAJWA CAF…

BAADA YA KUWAZIBUA HOROYA KIBABE….MAJINA YA MASTAA HAWA WA SIMBA YATAJWA CAF…

Habari za Simba SC

Vikosi vya Simba SC na Al Ahly ya Misri vinachuana vikali katika kinyang’anyiro cha kutoa mchezaji Bora wa wiki Ligi ya Mabingwa Afrika hatua ya Makundi Mzunguko wa 5.

Simba ambayo imeichapa Horoya mabao 7-0 wikiendi iliyopita katika Uwanja wa Benjamin Mkapa imetoa wachezaji wawili ambao ni Clatous Chama na Sadio Kanoute.

Clatous alifunga mabao matatu na kutoa pasi moja ya bao katika mchezo dhidi ya Horoya wakati Kanoute akifunga mabao mawili katika ushindi huo wa mabao 7.

Klabu ya Al Ahly ya Misri imetoa wachezaji wawili vile vile ambao walichangia ushindi wao wa mabao 4-0 dhidi ya Cotton Sport ambao ni washambuliaji Mahmoud Kahraba aliefunga mabao matatu dhidi ya Cotton Soprts na Percy Tau aliefunga bao 1.

Clatous Chama ndio mchezaji aliechaguliwa kuwa Mchezaji Bora wa Wiki mzunguko wa nne.

Hii ndio Orodha kamili ya wanaoshindania Mchezaji Bora wa Wiki;

SOMA NA HII  HII SASA KALI SIMBA YACHUKUA POINTI TATU NJE YA UWANJA