Home Uncategorized MSUVA ATUMA UJUMBE SENEGAL

MSUVA ATUMA UJUMBE SENEGAL


MSHAMBULIAJI nguli wa Taifa Stars, Simon Msuva amewataka Watanzania wote kutokuwa na wasiwasi na mchezo wa leo wa Afcon dhidi ya Senegal kwani wamejipanga vilivyo.

Taifa Stars leo saa 2 usiku itashuka uwanjani kupambana na Senegal katika mchezo wake wa kwanza katika fainali hizo utakaochezwa kwenye Uwanja wa 30 June huko nchini Misri.

Msuva ambaye ni winga za zamani wa Yanga ameliambia Spoti Xtra kuwa; 

“Jambo kubwa kwa Watanzania wenzangu ni dua zao ili tuweze kuwa na nguvu za tupambana kwa dakika zote 90 na kupata ushindi.”

SOMA NA HII  ILE ISHU YA RUSHWA INAYOMKABILI MAGUIRE NCHINI UGIRIKI