KOCHA Mkuu wa Azam FC, Rachid Taoussi amekiri ubora wa safu ya ushambuliaji wa Yanga na kuwa makini kutowapa nafasi ya kufanya mashambulizi.
Safu ya ushambuliaji ya Yanga inayoongozwa na Prince Dube, Jean Baleke, Kennedy Musonda, Clement Mzize, Pacome Zouzoua, Stephane Aziz Ki, Clatous Chama na Mudathir Yahya..
Kuelekea mchezo wa kesho dhidi ya Yanga, utakaochezwa uwanja wa Azam Complex uliopo Chamazi Dar-es-Salaam, Taoussi amesema ana matumaini ya kupata matokeo mazuri endapo wachezaji wake watatumia nafasi za wazi watakaozitengeneza.
“Yanga timu kubwa na wana kocha mzoefu, lengo la timu kucheza vizuri na kutafuta ushindi, wazuri kwenye kushambulia, tumefanyia kazi ubora huo na mapungufu yao kuyatumia kutafuta ushindi,” amesema .
Taoussi amesema wanakuwa makini kwa kuzuia mashambulizi ya wapinzani wao na kutumia nafasi wanazotengeneza kutafuta matokeo chanya dhidi ya Yanga.
SOMA NA HII NI PABLO...SIMBA YAWEKA REKODI YA AJABU....NABI ACHEKELEA MATOKEO..YANGA MAMBO YAMEIVA..