Home epl JURGEN KLOPP HATA HAELEWI SABABU YA BEKI WAKE ALEXANDER-ARNOLD KUACHWA

JURGEN KLOPP HATA HAELEWI SABABU YA BEKI WAKE ALEXANDER-ARNOLD KUACHWA


KOCHA Mkuu wa Klabu ya Liverpool, Jurgen Klopp amesema kuwa amepata mshtuko baada ya nyota wake Trent Alexender-Arnold kutojumuishwa kwenye kikosi cha timu ya taifa ya England.

Alexander-Arnold amewekwa kando kwenye timu ya taifa ya England na inaonekana kwamba hatakuwa sehemu ya kikosi ambacho kitakuwa kwenye harakati za kusaka tiketi ya kushiriki Kombe la Dunia katika mechi dhidi ya San Marino, Albania na Poland.

Klopp amesema kuwa bado hajaelewa maamuzi ya Kocha Mkuu wa England, Gareth Sothgate kwa kumuweka kando beki huyo.

Kwa sasa beki huyo amekuwa kwenye wakati mgumu uwanjani ambapo alikuwa kwenye janga la Corona jambo ambalo lilimfanya Klopp asiulize kwa nini aliachwa kwenye kikosi cha timu ya England, Novemba pia alikuwa anasumbuliwa na majeraha lakini kwa sasa anaonekana kuwa yupo fiti.

“Nimeshangazwa namna ambavyo hajatwa kwenye kikosi, sikuwa na mpango naye mkubwa katika msimu huu kwa kuwa niliamini kwamba angekuwa kwenye majukumu ya timu ya taifa, ila ajabu ni kwamba hajawa kwenye hicho kikosi jambo ambalo nimeshangaa.

“Huwa ninafanya maamuzi kila siku na inatokea kwamba watu wengine hawaelewi kile ambacho unakifanya. Ninaheshimu maamuzi ya Gareth ila sijaelewa sababu ya Alexaender-Arnold, bado ni kijana na ana uwezo pia,” 



SOMA NA HII  WAKATI JAHAZI LA MAN UTD LIKIWA HALIELEWEKI...RIO FERDINAND ATABIRI HAYA KUHUSU RONALDO...