Home Habari za michezo HUKU AKIENDELEA KUKAA BENCHI….HUSSEIN KAZI AVUNJA UKIMYA SIMBA….

HUKU AKIENDELEA KUKAA BENCHI….HUSSEIN KAZI AVUNJA UKIMYA SIMBA….

Habari za Simba leo

BEKI wa kati wa Simba, Hussein Kazi amesema kukaa benchi kunahitaji roho ngumu kwa kiu ya mchezaji yeyote ni kuona anacheza, lakini amekiri uwezo wa wachezaji wenzake wanaocheza nafasi hiyo kikosini kuwa wanastahili, huku akijipa moyo kuna siku naye atatumika kama kiu aliyonayo kwa muda mrefui.

Kazi amekuwa na wakati mgumu kutumika katika kikosi cha kwanza kutokana na Kocha Fadlu David kupenda kuwatumia zaidi Fondoh Che Malone, Abdulrazak Hamza na Chamou Karaboué, huku yeye akiishia kuwa benchi au jukwaani, huku akikiri bado hajakata tamaa anasubiri zamu yake ifike.

“Najua kuna mechi nyingi za Kombe la Shirikisho Afrika (FA), FA, Ligi Kuu ikifika zamu yangu nitacheza kama ilivyo kwa wenzangu ambao wanapata nafasi kwa sasa, kikubwa wanaisaidia timu kufanya vizuri,” alisema beki huyo aliyesajiliwa msimu uliopita akitokea Geita Gold na kuongeza;

“Ushindani ni mkali ukipata nafasi ukashindwa kufanya vizuri, ujue kuna wenzako ambao walikuwa wanaisubiri kwa hamu na ni kitu kizuri kwenye timu kushindania namba.”

Alisema anachoshukuru ni kwamba kocha Fadlu kuna vitu amekuwa akimwambia avifanyie kazi, ili kupunguza makosa na kupata nafasi kwenye mechi zijazo, hivyo anapambana kuhakikisha anatekeleza kama inavyopaswa.

“Ligi ya msimu huu ni ngumu sana, yapo baadhi ya makosa madogo ninayoyafanyia kazi na kocha amekuwa akiniambia kipi nikifanye ili niwe bora, ndio maana nasema kazi hii inahitaji moyo mgumu, kwani kuna wakati unatamani kucheza ila inakuwa ngumu,” alisema Kazi.

SOMA NA HII  YAO NA SOMO KWA WAZAWA MAMBO YAPO HIVI