Home Habari za michezo WABABE WA YANGA KUKUTANA USO KWA USO….ISHU NZIMA HII

WABABE WA YANGA KUKUTANA USO KWA USO….ISHU NZIMA HII

habari za yanga-NABI

HUKO mtaani kama unataka kuwakata stimu mashabiki na wapenzi wa Yanga kukumbushia vipigo viwili mfululizo vilivyoitibulia timu hiyo katika Ligi Kuu Bara.

Kama umesahau, baada ya Yanga kucheza mechi nane mfululizo bila kupoteza wala kuruhusu bao lolote, ilifyatua na Azam kwa kufungwa bao 1-0 kisha Tabora United ikaja kutonesha kidonda kwa kuinyoosha mabao 3-1, sasa timu hizo kesho jioni zinakutana kwenye Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi, mjini Tabora.

Nani atakayemtibulia mwenzake? Hilo ndilo swali linalosubiriwa kutenguliwa katika pambano hilo la Ligi Kuu wakati Azam inayoongoza msimamo kwa sasa itakapokuwa ugenini kuvaana na Nyuki wa Tabora, huku rekodi zikionyesha msimu uliopita kwenye uwanja huo zilitoka suluhu baada ya awali Azam kushinda 4-1 huku wapinzani wao wakiwa pungufu.

Tabora inayoshikilia nafasi ya tano ikiwa na pointi 21, tisa pungufu na zile ilizonazo Azam iliyopo kileleni na kesho utakuwa ni mtihani kwa pande zote, huku mtihani zaidi ukiwa upande wa Tabora inayohitaji ushindi ili kuboresha nafasi yao, lakini Azam, ikiwa na safu bora, ina matumaini ya kuongeza pointi tatu muhimu.

Azam inayonolewa na kocha Rachid Taoussi, imekuwa na mwenendo mzui hadi sasa, ikiwa imeshinda mechi saba mfululizo.

Taoussi amekuwa na mafanikio kwa kuunda mfumo wa ushambuliaji wenye ufanisi na safu ya ulinzi imara.

Matajiri hao wa Chamazi wanajivunia wachezaji wenye uwezo mkubwa wa kufunga, akiwemo Feisal Salum aliyehusika katika mabao nane, akiwa na mabao manne na asisti nne, Nassoro Saadun pia amefunga mabao manne na ushirikiano katika safu ya mbele umekuwa ni tishio kwa timu nyingi za Ligi Kuu.

Kwa upande wa Tabora chini ya kocha Anicet Kiazmak, imeonyesha kiwango kizur akijivunia umoja wa wachezaji hasa Yacouba Songne na Heritier Makambo waliohusika mabao 12 kati ya 16 yaliyofungwa na timu yao.

Nyota hao wote waliwahi kuitumikia Yanga wamekuwa pacha tishio katika hiyo kwa kufunga na kuasistiana katika mechi kadhaa zilizopita, Yacouba akiwa na mabao manne na asisti tatu wakati Mzee wa Kuwajaza akifunga mabao mawili na asisti tatu.

Historia ya mechi kati ya timu hizi inaonyesha Azam imekuwa na ufanisi zaidi. Msimu uliopita, Azam ilishinda mechi ya kwanza kwa mabao 4-0 kwenye uwanja wa Azam Complex, ambapo Feisal Salum alifunga hat-trick, lakini mechi ya pili ilimalizika kwa suluhu.

Katika mchezo huu, Azam itahitaji ushindi ili kujizatiti kileleni mwa ligi na kufikisha pointi 33, na hivyo kuendelea kutawala msimamo. Kwa upande wa Tabora, ushindi utawafanya kujipatia pointi muhimu na kuwa karibu na nafasi ya nne, ambayo inashikiliwa na Singida Black Stars.

Kocha wa Azam, Taoussi alisema: “Tunajivunia safu yetu ya ushambuliaji licha ya changamoto tulizonazo, lakini hatutegemei tu mabao kutoka kwa Feisal au Nassoro.

Tunahitaji kila mchezaji kufanya kazi kwa bidii na kuzuia makosa katika sehemu ya ulinzi. Tabora ni timu imara na tunaheshimu uwezo wao, lakini tunakwenda uwanjani kutafuta pointi tatu muhimu ili kuendelea kujizatiti kileleni.”

Kwa upande wa kocha wa Tabora, kocha Anicet alisema: “Azam ni timu nzuri na tuna heshima kubwa kwao, lakini sisi pia tumethibitisha kuwa tunaweza kupambana na timu kubwa.

Wachezaji wangu wa mbele, Yacouba na Makambo, wameshinda mapambano mengi na tunatumaini kuwa wataendelea kuwa na mchango mkubwa. Tunahitaji kufanya kazi kwa umoja na kutumia kila nafasi ili tushinde mechi hii.”

Mechi nyingine itakayopigwa kesho jioni ni kati ya Fountain Gate itakayokuwa wenyeji wa Coastal Union kwenye Uwanja wa Tanzanite Kwaraa uliopo Manyara.

Fontain itashuka uwanjani ikiendelea kuwategemea nyota wake, Seleman Mwalimu na Edger William ambao wanaongoza orodha ya waliotupia mabao mengi hadi sasa, lakini Coastal nayo ikitambia ni Maabad Maulid, John Makwata na David Semfuko ambao wameiwezesha timu hiyo kuanza kurudi katika mstari baada ya awali kuanza vibaya ligi chini ya Mkenya David Ouma aliyetimuliwa na kumpisha Juma Mwambusi.

SOMA NA HII  WEEKEND INAKUJA NA MAOKOTO NAYO YANAZIDI KUONGEZEKA...WEKA MKEKA WAKO HAPA..