Mwisho wa msimu yeye na Djuma Shaban wakaachwa. Yeye alikuwa na mkataba mkononi na Yanga walitumia nafasi kupata kiasi cha Sh100 milioni kutoka kwa Azam. Kuondoka kwake kuliwashangaza wengi. Ni kwa sababu tu mashabiki wa Yanga walimuamini Injinia Hersi Said na maamuzi yake, lakini ni namna gani ungeweza kuachana na Wacongo hawa. Djuma na Bangala.
mwingine?
Lakini vile vile rafiki yangu Bangala kama hawezi kupata timu Afrika Kaskazini anaweza kupata timu wapi? Tanzania imekuwa ikitoa mishahara mizuri kwa wachezaji wa kigeni. Hizi timu zetu tusizichukulie poa. Zimekuwa zikitoa mishahara mizuri kwa wachezaji wake na ndiyo maana wengi wapo hapa.