Home Habari za michezo KUELEKEA MECHI NA FOUTAING GATE KESHO…..MAPYA KWA YANGA HAYA HAPA πŸ‘€πŸ‘€..

KUELEKEA MECHI NA FOUTAING GATE KESHO…..MAPYA KWA YANGA HAYA HAPA πŸ‘€πŸ‘€..

Habari za Yanga leo

NYASI za Uwanja wa KMC Complex, Mwenge zitawaka moto kwenye mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara kesho, ambapo Yanga itawakaribisha Fountain Gate, kila mmoja akihitaji kuvana alama tatu.

Yanga inashika nafasi ya pili wakiwa na alama 36 wakiwa tayari wamecheza mechi 14, wanawakaribisha Fountain Gate FC, wanashika nafasi ya sita wakiwa na alama 20 kwa michezo 16 ya ligi hiyo.

Kuelekea mchezo huo makocha wa timu zote mbili wametambia kila mmoja akihitaji alama tatu, kwa mwenyeji wa mchezo huo, Sead Ramovic amesema wamepata muda mzuri kwa kujiandaa na tayari wamewasoma wapinzani wao.

β€œKiukweli ni wapinzani wagumu lakini kwa ukubwa wa timu hii pamoja na maandalizi yetu tupo tayari kujitoa kwa asilimia mia moja ili kukusanya alama tatu, Kila mchezo huja na maandalizi tofauti, kwa kuwa malengo yetu kesho kushinda basi tumejiandaa kucheza mchezo nzuri na kutengeneza nafasi za kutupa alama tatu,” amesema.

Ramovic amesema hawatatazama kabisa matokeo ya mechi zilizopita zao na wapinzani wao kwa sababu kila kila mchezo unakuwa na mipango tofauti na michezo ya nyumbani ambayo wameshacheza.

β€œNiwaombe wananchi waje kutusapoti siku ya kesho kwa sababu tunawahitaji sana,” amesema Kocha huyo ambaye anaamini alama hizo zitafikia malengo yao ya kuhitaji kurejea katika nafasi yao ya kuongoza ligi hiyo.

Kocha wa Fountain Gate, Mohammed Muya amesema ameandaa kikosi chake ikiwemo sehemu ya ulinzi ambayo imekuwa ikifanya makosa kwa kuruhusu bao katika michezo ya hivi karibuni.

β€œTunafahamu ubora wa Yanga wako vizuri lakini wana mapungufu yao nafasi ya ulinzi ipo vizuri, tumejimarisha tukiruhusu mabao mengi na timu za hapa mjini, sasa hivi tunaomba huyo jinamizi la kuruhusu mabao mengi na timu za Dar es Salaam Mungu atuondolee,” amesema Muya.

SOMA NA HII  KAZI INAENDELEA, MCHAKATO WA KUMPATA MRITHI WA KAZE UMEFIKIA HAPA