Home Habari za michezo KISA DIARRA….CAMARA ‘SPIDER’ APEWA TUZO YAKE MAPEAAA 🤗🤗…

KISA DIARRA….CAMARA ‘SPIDER’ APEWA TUZO YAKE MAPEAAA 🤗🤗…

Habari za Michezo

WAKATI Ligi Kuu Bara ikiwa ndio kwanza imeanza duru la pili na ikienda kusimama hadi Januari 20 mwakani, aliyekuwa kipa wa Coastal Union, Ley Matampi ameitoa tuzo ya Kipa Bora msimu huu kwa Moussa Camara ‘Spider’, akiamini ndiye mrithi wake kwa sasa baada ya yeye kuondoka.

Matampi alitwaa tuzo hiyo msimu uliopita kwa kuwa na ‘clean sheets’ 15 akimbwaga aliyekuwa mtetez, Diarra Djigui wa Yanga aliyemaliza na 14, lakini hivi karibuni alitemwa na Coastal Union, na kwa mtazamo wake amesema licha ya kwamba ligi bado ni mbichi, lakini anaamini Camara wa Simba ndiye atakayetwaa msimu huu.

Kipa huyo Mkongomani alisema anaona mambo yakimnyookea Spider ambaye kabla ya mechi ya jana ya timu ya Simba dhidi ya Singida Black Stars alikuwa akiongozwa kwa clean sheet 11 kupitia mechi 14, kitua ambacho Matampi anaona hakuna wa kumzuia msimu huu kutwaa tuzo hiyo ikizingatiwa Diarra ni majeruhi.

“Camara atanufaika na makosa ya makipa wengine wanaoendelea kuruhusu mabao, pia majeraha aliyoyapa Diarra yanayomfanya kukosa mechi kadhaa kwa sasa. Simba inacheza kwa hesabu sana si kwamba haifanyi makosa, lakini inahitaji kukutana na timu yenye makali itakayowalazimisha kufanya makosa,” alisema.

“Camara ni kipa anayepanga vizuri mabeki, ndio maana amekuwa na wakati rahisi akiwa langoni. Pia huwezi kuacha kuisifu safu hiyo ya ulinzi kwa umakini na ubora unaozidi kumsogeza Camara katika kubeba tuzo hiyo,” aliongeza Matampi aliyewahi kutamba na TP Mazembe, DC Motema Pembe, FC Lupopo na nyingine.

Camara, raia wa Guinea tangu ametua Simba akitokewa AC Horoya msimu huu amekuwa na rekodi nzuri ndani ya kikosi hicho huku akiwakalisha benchi makipa Ali Salum, Aishi Manula, Ayoub Lakred na Hussein Abel kutokana na kuaminiwa na kocha Fadlu Davids, aliyemtumia katika mechi 14 za Ligi kwa dakika 1260.

SOMA NA HII  RIPOTI: HIVI NDIVYO YANGA 'WALIVYOTUMBUA' BIL 22 KUPATA UBINGWA WA LIGI NA FA...