Home Habari za michezo AHMED ALLY:- TUKISHINDA KESHO UBINGWA HUU HAPA….TUTAANDA SHEREHE MAPEMA….

AHMED ALLY:- TUKISHINDA KESHO UBINGWA HUU HAPA….TUTAANDA SHEREHE MAPEMA….

MSEMAJI SIMBA AINGIA MATATANI...

UONGOZI wa klabu ya Simba umesema kutokana na ugumu na umuhimu wa mchezo dhidi ya Azam FC, wamevunja utaratibu wao wa kuwaruhusu wachezaji kwenda nyumbani kupumzika kila wanapomaliza mechi.

Simba waliingia kambini moja kwa moja kwa maandalizi ya mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Azam FC, utakaochezwa kesho Jumatatu, Februari 24, Uwanja wa KMC Complex uliopo Mwenge.

Meneja wa idara ya habari na mawasiliano wa Simba, Ahmed Ally amesema baada ya mchezo na Namungo FC kikosi kiliingia kambini moja kwa moja tofauti na ilivyozoeleka wanapomaliza mechi wachezaji wanapata mapumziko ya siku moja.

“Hii mechi muhimu Azam FC ni timu ngumu imefanya usajili mzuri wa wachezaji wake, inatulazimu kuvunja utaratibu wetu tuliojieekea baada ya mechi wachezaji wanaenda nyumbani kwa mapumziko huu mchezo ni sehemu ya njia yetu ya kuelekea ubingwa msimu huu.

“Laiti tunapata matokeo mazuri dhidi ya Azam FC basi tunakaribia walau nusu ya safari yetu ya kuelekea kwenye ubingwa,” amesema.

Ahmed amesema wanafanya maandalizi makubwa yenye umakini , kuhakikisha wanapata ushindi dhidi ya Azam FC ili Simba ianze kuandaa sherehe za ubingwa.

SOMA NA HII  ILE ISHU YA STRAIKA HATARI WA SIMBA QUEENS KWENDA ULAYA IKO HIVI...UONGOZI WAFUNGUKA...