Home Habari za michezo ATEBA, AHOUA WAJIPATA SIMBA….FADLU AWAPA UHAKIKA WA MAISHA….JUKUMU LAO JIPYA HILI….

ATEBA, AHOUA WAJIPATA SIMBA….FADLU AWAPA UHAKIKA WA MAISHA….JUKUMU LAO JIPYA HILI….

Habari za Simba leo

KOCHA Mkuu wa Simba, Fadlu Davids amebainisha kuwa Jean Charles Ahoua na Leonel Ateba watakuwa na jukumu la kupiga penati wanapokuwa uwanjani katika michezo mbalimbali.

Kauli Kocha Fadlu ameitoa baada ya kutamatika kwa dakika 90 za mchezo wa Namungo wa Ligi Kuu Tanzania Bara baada ya Simba kupata penati tatu kati ya hizo wamepata mbili na kukosa moja.

Katika mchezo huo Simba ilishinda mabao 3-0, kati ya mabao hayo mawili ya penati ambayo ameyafunga Jean na penati moja wamekosa iliyopigwa na Ateba.

Kitendo cha Ateba kukosa penati hiyo, Kocha Fadlu amesema hawezi kumtupia lawama Ateba kwa kukosa anaamini haikuwa bahati kwao na hata wangepata penalti ya nne angepiga.

“Hajali kati ya Ahoua na Ateba nani anapiga penati , anaweza kuchukuwa ya kwanza na tatu Ahoua, pili na nne Ateba, kwa sababu wanamaelewano mazuri,” amesema.

Aidha,Fadlu amesema nyota hao wamepewa jukumu hilo na kulifanyia kazi vizuri licha ya Ateba kukosa penati moja, kikubwa wamecheza vizuri na kupata ushindi wa mabao 3-0 na kurejea na pointi tatu.

Kesho Simba itashuka tena uwanjani kukipiga na Azam FC mchezo utakaochezwa kwenye uwanja wa Mkapa Jijini Dar Es Salaam kuanzia saa moja usiku.

SOMA NA HII  KUELEKEA AFCON:-UKIACHA UWANJA MPYA ARUSHA....VIWANJA HIVI VIPYA KUJENGWA NCHINI...