Home Habari za michezo BAADA YA YANGA KUMBEBA MILOUD ‘KIBABE’….SINGIDA WAFANYA ‘KUFRU’ NYINGINE…KOCHA MPYA HUYU HAPA..

BAADA YA YANGA KUMBEBA MILOUD ‘KIBABE’….SINGIDA WAFANYA ‘KUFRU’ NYINGINE…KOCHA MPYA HUYU HAPA..

Habari za Michezo

UONGOZI wa Singida Black Stars umemtambulisha kocha Juan Carlos Oliva (MAGRO) kutoka Hispania kuwa kocha msaidizi namba moja kuongeza nguvu benchi lao la ufundi akishirikiana na Davis Ouma.

Ujio wa Juan ni kwenda kushirikiana na Ouma baada ya kuondoka kwa kocha wao Mkuu, Hamdi Miluod aliyejiunga na Yanga akichukua nafasi ya Sead Ramovic aliyetimkia CR Belouizdad ya Morocco.

Hatua ya Singida Black Stars kumtambulisha kocha namba moja msaidizi ni baada ya kukubaliana na maamuzi ya Yanga ambao walimchukua kocha Hamdi ambapo Singida walidai Yanga haikufuata utaratibu wa kumchukua mwalimu huyo anayekinoa kikosi cha Yanga.

Taarifa kutoka Singida Black Stars, imeeleza kuwa wameamua kufanya maboresho ya benchi la ufundi na kuongeza nguvu, mabadiliko hayo wamemrejesha kundini aliyekuwa mshambuliaji wao, Amisi Tambwe kuwa meneja wa timu na Fredy Chalamila amehamishiwa nafasi ya Mratibu Mkuu.

Kocha Juan amewahi kufundisha timu mbalimbali barani Ulaya na Asia na baadhi ya timu hizo ni Unió Esportiva Lleida, Deportivo Alaves, Aris Salónica, Villarreal B, Salamanca, Nástic de Tarragona, Aris de Salónica za Hispania, Sharjah FC (Falme za Kiarabu), Al-Ahly na Al-Ain, za Saudia Arabia.

SOMA NA HII  JUKUMU LA KUIDONDOSHA SIMBA WAPEWA MASTAA HAWA YANGA