Home Habari za michezo WAKATI CHAMA , AZIZI KI WAKING’ARA JUZI….PACOME AVUNJA UKIMYA KUHUSU YANGA…

WAKATI CHAMA , AZIZI KI WAKING’ARA JUZI….PACOME AVUNJA UKIMYA KUHUSU YANGA…

Habari za Yanga Leo, Aziz KI

KIUNGO wa Yanga, Pacome amesema kuwa hesabu kubwa ni kupata pointi kwenye mechi ambazo wanacheza uwanjani wakiwa hawana muda wakupoteza kwa sasa.

Katika mchezo dhidi ya Mashujaa uliochezwa Uwanja wa Lake Tanganyika, mwisho wa reli Kigoma, baada ya dakika 90 ubao ulisoma Mashujaa 0-5 Yanga huku Pacome akichaguliwa kuwa mchezaji bora wa mchezo na alitoa pasi mbili kwenye mchezo huo waliposepa na pointi tatu mazima.

Mbali na Pacome kutoa pasi mbili kiungo mshambuliaji wa Yanga, Clatous Chama alifunga mabao mawili kwenye mchezo huo akianzia benchi ugenini alichukua nafasi ya Aziz Ki.

Pacome amesema: “Kila mchezo kwetu ni muhimu na hakuna muda wakupoteza, tunajua ushindani ni mkubwa nasi tunapambana kuwa bora kupata matokeo uwanjani kwenye mechi ambazo tunacheza kila wakati.”

Yanga ni vinara wa ligi wakiwa na pointi 55 baada ya mechi 21 kinara wa kucheka na nyavu ni Prince Dube na Clement Mzize hawa wametupia mabao 10 kila mmoja ndani ya msimu wa 2024/25 na Pacome katupia mabao 7.

SOMA NA HII  SIMBA SC KUSHUSHA WACHEZAJI HAWA SITA NA KUKAMILISHA USAJILI WAKE MSIMU HUU