Home Habari za michezo HUKO YANGA HAWACHEKI NA WOWOTE AISEEE 😎….NI MWENDO WA ‘MAPANGA SHAAA’…

HUKO YANGA HAWACHEKI NA WOWOTE AISEEE 😎….NI MWENDO WA ‘MAPANGA SHAAA’…

Habari za Yanga leo

YANGA hawacheki na wowote huko ni spidi ndefu kila kona kutokana na rekodi ambazo zinaandikwa na wachezaji wao uwanjani katika eneo la kufunga na kutoa pasi za mabao, iwe wameanza kikosi cha kwanza ama wameanzia benchi.

Mchezo dhidi ya Mashujaa uliochezwa Uwanja wa Lake Tanganyika, Februari 23 2025 baada ya dakika 90 ubao ukasoma Mashujaa 0-5 Yanga, Clatous Chama akianzia benchi alifunga mabao mawili baada ya kuingia akichukua nafasi ya Aziz Ki na kufikisha jumla ya mabao matatu kwenye ligi akiwa na pasi mbili za mabao.

Wakati akiwa amehusika katika mabao matano kati ya 55 kuna mshambuliaji Prince Dube huyu kahusika katika mabao 17 akiwa ni namba moja kwa mastaa waliohusika katika mabao mengi zaidi.

Ni mabao 10 kafunga na pasi 7 za mabao huku kwa upande wa Simba ni Jean Ahoua kahusika katika mabao 16 akifunga mabao 10 na pasi 6 za mabao. Ikumbukwe kwamba Dube ni mchezaji wa kwanza kufunga hat trick ilikuwa kwenye mchezo dhidi ya Mashujaa, Uwanja wa KMC Complex.

Kila kona kwa sasa Yanga wanakimbiza ndani ya ligi namba nne kwa ubora ambapo ushindani unazidi kuongezeka kila leo ndani ya uwanja kwa mechi ambazo zinachezwa uwanjani.

Baada ya mechi 21 ambazo ni dakika 1,890 safu ya ushambuliaji ya Yanga ni namba moja ikiwa imekusanya jumla ya mabao 55 ni wastani wakufunga bao moja kila baada ya dakika 34 ndani ya uwanja ambapo pointi zao kibindoni pia ni 55.

Wamekuwa kwenye mwendo wa 55 na mchezo wao uliopita walipata ushindi mkubwa wa mabao 5-0 dhidi ya Mashujaa ambayo imetangaza kuachana na kocha wao Mohamed Abdallah Bares ambaye alikuwa benchi kwenye mchezo uliopita dhidi ya Yanga na mchezo wake wa mwisho kukaa benchi ilikuwa ni Februari 26 ubao wa Uwanja wa Liti ulisoma Singida Black Stars 3-0 Mashujaa.

SOMA NA HII  SAKATA LA GSM KUDHAMINI ZAIDI YA TIMU MOJA..SENZO AFUNGUKA..ADAI NI UJINGA..ATOA LAANA...