Home Habari za michezo KISA SIMBA…YANGA KULIPA MAMILIONI YA PESA FIFA….BARUA YATUA KWA MABOSI TFF….

KISA SIMBA…YANGA KULIPA MAMILIONI YA PESA FIFA….BARUA YATUA KWA MABOSI TFF….

Habari za Yanga leo

MASHABIKI wa Simba wanachekelea hatua ya mchezo dhidi ya Yanga kuahirishwa, wanawatambia wenzao wa Yanga, kwamba mechi itapangwa, mtapigiwa simu moja tu kutoka juu na mtacheza, lakini wasichojua ni kwamba Wananchi hawatanii na wamejipanga kwa vita mpya, wakikubali kutumia Sh121 milioni kuitafuta haki FIFA.

Unaposoma taarifa hii tambua kwamba, Yanga imeshaweka kila kitu sawa kufungua kesi rasmi katika Mahakama ya Kimataifa ya Usuluhishi wa Masuala ya Michezo (CAS), huku wakitenga mamilioni hayo.

Kufungua tu kesi CAS inahitajika uwe umeweka kiasi cha Dola 46,000 (Sh121 Milioni ) ambazo tajiri wa Yanga ameshaziingiza kwenye akaunti za Yanga zitumwe haraka ili wapiganie heshima wanayoidai.

Inafahamika kuwa kuna juhudi zimekuwa zikifanywa ili kuirudisha Yanga mezani kwa mazungumzo, lakini mabosi wa klabu hiyo wanavikimbia vikao wakihofia msimamo wa mashabiki wao ambao hawataki kusikia suluhu yoyote mezani na Bodi ya Ligi pamoja na Shirikisho la Soka (TFF).

Msimamo huo wa mashabiki umeonyeshwa hadharani juzi, wakati klabu hiyo ilipotuma salamu za pongezi kwa Rais wa TFF pamoja na CECAFA, Wallace Karia wakimpongeza kwa hatua ya kushinda kuwa Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Soka Afrika (CAF).

Baada ya salamu hizo zilizotumwa katika mtandao wa Instagram, mashabiki wa timu hiyo walikuwa wakali walitoa lugha kali na kuifanya Yanga kuondoa salamu hizo kwa ajili ya kuheshimu msimamo wa mashabiki na wapenzi wa timu hiyo waliochukizwa kwa Dabi ya Kariakoo kuahirishwa kiutata Machi 8, 2025.

WANASHERIA 9 MEZANI

Ingawa Yanga haitaki kulizungumzia hilo hadharani, lakini inafahamika kuna jopo la wanasheria tisa limeshajiandaa kwa uwasilishwaji wa shauri hilo.

Hatua ya Yanga kufungua kesi huyo ni kufuatia Bodi ya Ligi Tanzania (TPLB) na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), kutotoa majibu ya barua ya klabu hiyo iliyotoa masaa 72 ambayo yalifikia tamati jana mchana.

Yanga inapinga hatua ya Bodi ya Ligi kuuahirisha mchezo dhidi ya Simba uliotakiwa kuchezwa Machi 8 kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam bila kuzingatia kanuni zinazosimamia Ligi.

Hakuna kiongozi wa Bodi wala wa TFF waliopatikana kuelezea juu ya masharti ya barua ya Yanga, ingawa inafahamika kuwa kuna barua hiyo ilishatua mezani kwa Mtendaji Mkuu wa Bodi, Almasi Kasongo.

SOMA NA HII  MKUDE AIBUA 'ZONGO' TIMU YA TAIFA....KOCHA TAIFA STARS AULIZWA MASWALI MAGUMU...