Home Azam FC AZAM vs YANGA…..HIZI HAPA ‘SAPRAIZI’ ZA KIBABE ZINAZOWEZA KUTOKEA….AZIZI KI NDANI….

AZAM vs YANGA…..HIZI HAPA ‘SAPRAIZI’ ZA KIBABE ZINAZOWEZA KUTOKEA….AZIZI KI NDANI….

Yanga sc

KIPUTE cha leo pale Azam Complex kimeshikilia mambo mawili makubwa; mosi, ni je Yanga itashinda na kukomaa juu ya msimamo huku ikiipoteza kabisa Azam katika mbio za ubingwa wa Ligi Kuu Bara au Azam itashinda na kuipunguza kasi Yanga katika mbio za kuwania ubingwa huo.

Lakini, kuna mambo mengine yanayoendelea upande wa mechi zingine za ligi hiyo ikiwamo timu zinazopigania kutishuka daraja na zile zinazopambana kuhakikisha kwamba zinapenya na kuingia katika Top Four ili kupata nafasi ya kuiwakilisha Tanzania kimataifa.

Lakini, habari njema kwa wapenzi na mashabiki wa Yanga ni kwamba leo kuna uwezekano mkubwa Stephane Aziz Ki akaikabili Azam baada ya kukosekana katika mechi mbili mfululizo zilizopita kutokana na kutokuwa fiti huku maumivu ya mgongo yakitajwa kumsumbua.

Aziz Ki ambaye mara ya mwisho alitokea benchini Machi 29 mwaka huu wakati Yanga ikiifunga Songea United mabao 2-0 kwenye mechi ya Kombe la Shirikisho (FA) hatua ya 16 bora, alikosekana katika mechi mbili zilizopita za ligi ambazo Yanga ilizifunga Tabora United (3-0) na Coastal Union (1-0).

Alhamisi hii, Yanga itakuwa ugenini kuikabili Azam katika mchezo wa Ligi Kuu Bara utakaochezwa kwenye Uwanja wa Azam Complex, Dar kuanzia saa 1:00 usiku huku ikiikosa huduma ya kiungo wake mkabaji, Khalid Aucho ambaye anasumbuliwa na majeraha ya misuli ya paja.

Aziz Ki alisema kwa sasa anaendelea vizuri na kukosa kwake mechi zilizopita kusiwatishe mashabiki bali wawe na amani kwani licha ya kutocheza alikuwa akifanya mazoezi.

“Nafanya mazoezi madogo madogo ya kuuweka mwili sawa, hivyo natumaini nitaweza kucheza hata mechi zijazo kwani tayari nitakuwa kwenye utimamu wangu.

“Mechi zilizopita sikufanikiwa kucheza, lakini nilikuwa nafanya mazoezi kama kawaida, hivyo muda wowote mashabiki wategemee kuniona kazini,” alisema Aziz Ki ambaye msimu uliopita alikuwa mfungaji bora wa Ligi Kuu Bara akifunga mabao 21.

Kiungo huyo ambaye huu ni msimu wake wa tatu kuitumikia Yanga, amekuwa na rekodi nzuri ya kuifunga Azam kwani mara tano alizokutana nayo kwenye ligi amefunga mabao manne ikiwemo hat trick moja.

Kwa ujumla, Aziz Ki amecheza dhidi ya Azam mara tisa kwenye michuano tofauti, akifunga mabao sita ambapo manne kwenye ligi na mawili Ngao ya Jamii, huku akishindwa kufunga katika Kombe la FA. Kwenye ligi, Aziz Ki amecheza dhidi ya Azam mara tano, FA (2) na Ngao ya Jamii (2).

SOMA NA HII  BAADA YA KUTAKATA CHINI YA NABI....'BACCA' KAANGALIA UPEPO WA MSIMU UJAO YANGA..KISHA AKASEMA HAYA...