Home Habari za michezo HIZI HAPA NONDO ‘KUNTU’ ZA BOSS WA MAN UNITED NA RAIS SAMIA….ACADEMY...

HIZI HAPA NONDO ‘KUNTU’ ZA BOSS WA MAN UNITED NA RAIS SAMIA….ACADEMY KUJENGWA….

Habari za Michezo

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan leo Ijumaa, Aprili 11, 2025 amekutana na mmiliki wa Manchester United, Sir Jim Ratcliffe, ikulu, Dar es Salaam.

Katika kikao hicho, Rais Samia na Ratcliffe wamefanya mazungumzo ya ushirikiano katika masuala ya utalii na michezo.

“Katika mazungumzo yao Rais Samia amemshukuru Sir Jim Ratcliffe kupitia Taasisi yake ya Six Rivers ambayo ina shughulika na masuala ya Uhifadhi, kwa namna inavyofanya vizuri katika kudhibitimuingiliano wa wanyamapori na binadamu kwa kushirikiana na Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) pamoja na Taasisi ya Utafiti wa Wanyamapori Tanzania (TAWIRI).

“Kupitia Taasisi yake ya Six Rivers, Sir Jim Ratcliffeamebainisha kuwa Taasisi hiyo imedhamiria kurejesha hadhiya Hifadhi ya Taifa ya Selous na kuwa na Wanyama wakubwa katika Hifadhi hiyo,” imesema taarifa ya Ikulu.

Kukutana huko kwa Ratcliffe na Rais Samia ni kutimia kwa ahadi ambayo bosi huyo wa Man United aliitoa Februari mwaka huu ya kuja nchini pindi alipokutana na katibu mkuu wa wizara ya maliasili na utalii, Dk Hassan Abbasi.

Katika mazungumzo hayo ya leo, Ratcliffe amemkabidhi rais Samia, zawadi ya jezi ya Manchester United ambayo imesainiwa na wachezaji wa timu hiyo.

Kwa upande wake Rais Samia, amemkabidhi Ratcliffe zawadi ya picha pamoja na Jezi ya Timu ya Taifa Tanzania (Taifa Stars) yenye ujumbe wa, “Amaizing Tanzania”

Aidha katika taarifa hiyo, Rais Samia amemtaka mmiliki huyo wa Man United kuangalia uwezekano wa timu yake kujenga vituo vya kuendeleza vipaji vya wachezaji vijana nchini.

SOMA NA HII  BAADA YA KUPONYEA DIRISHANI KUSHUKA DARAJA MSIMU HUU...MTIBWA SUGAR WAFUNGUKA WALICHOIFANYIA TZ PRISON...