Home Habari za michezo KUELEKEA MECHI YA SIMBA NA WASAUZI…..HILI HAPA JIPYA KUTOKA KWA ‘SEMAJI LA...

KUELEKEA MECHI YA SIMBA NA WASAUZI…..HILI HAPA JIPYA KUTOKA KWA ‘SEMAJI LA CAF’….

Habari za Simba leo

MENEJA wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Simba, Ahmed Ally, ameweka bayana dhamira ya klabu hiyo kuandika historia mpya katika michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika, wakilenga kuvuka hatua ya nusu fainali dhidi ya Stellenbosch FC ya Afrika Kusini.

Katika mahojiano maalum, Ahmed amesema kuwa Simba imejifunza kutokana na makosa ya nyuma walipokutana na vigogo wa Afrika Kusini kama Kaizer Chiefs na Orlando Pirates, walishindwa kuendelea zaidi ya robo fainali. Lakini kwa msimu huu, wamejipanga kuhakikisha wanafika mbali zaidi.

“Makosa ya nyuma yametufundisha. Safari hii tumejipanga kwa umakini mkubwa kwa sababu dhamira yetu ni kucheza fainali, Timu imeimarika, hasa inapokuwa ugenini,” amesema.

Simba itaingia kwenye mchezo wa marudiano utakaopigwa Jumapili, Aprili 27 katika Uwanja wa Moses Mabhida, Durban, ikiwa na faida ya bao 1-0 walilopata katika mchezo wa kwanza uliofanyika New Amaan Complex, Zanzibar.

Ahmed ameeleza kuwa rekodi nzuri ya Simba wakiwa ugenini ni moja ya nguzo za matumaini yao. Alitolea mfano wa mechi dhidi ya Al Masry walipofungwa 2-0 lakini bado wakapambana kwa ubora mkubwa na kuwatikisa wapinzani wao kisaikolojia.

“Simba hii ni tofauti. Tuna historia ya kupambana bila woga ugenini, kuanzia dhidi ya Al Ahly Tripoli hadi Al Masry. Sasa tunakutana na Stellenbosch, tunaamini tunaweza kwenda kwao na kupata matokeo tunayotaka,” amesema.

Kwa mashabiki wa Simba, matumaini ni makubwa kuona timu yao ikiweka historia kwa kufuzu fainali ya Kombe la Shirikisho kwa mara ya kwanza, huku wakiamini kuwa dhamira, maandalizi na morali ya kikosi chao msimu huu ni silaha tosha kufanikisha hilo.

SOMA NA HII  MASHINE HII HAPA.....YANGA WAITIBULIA AS VITA DILI LA KUMPATA....WAMTUMIA MKATABA 'CHAP' HARAKA...