Home Habari za michezo DAKIKA CHACHE BAADA YA KUTINGA FAINAL CAF….RAIS SAMIA ATIA ‘NGUVU’ SIMBA….

DAKIKA CHACHE BAADA YA KUTINGA FAINAL CAF….RAIS SAMIA ATIA ‘NGUVU’ SIMBA….

Habari za Simba leo

TIMU ya Simba imefanikiiwa kwenda Fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika baada ya sare ya bila kufungana na wenyeji, Stellenbosch katika mchezo wa marudiano wa Nusu Fainali jioni ya leo Uwanja wa Moses Mabhida Jijini Durban, Afrika Kusini.

Simba wananufaika na ushindi wa 1-0 kwenye mchezo wa kwanza wa Jumapili iliyopita Uwanja wa New Amaan Complex, Zanzibar, bao pekee la kiungo wa Muivory Coast, Jean Charles Ahoua dakika ya 45’+2.

Simba sasa inasubiri mshindi wa jumla kati ya RSB Berkane ya Morocco na CS Constantine ya Algeria ambazo zinarudiana leo kuanzia Saa 1:00 usiku Uwanja wa Mohamed-Hamlaoui Jijini Constantine.

Ikumbukwe RSB Berkane ilishinda 4-0 kwenye mchezo wa kwanza mabao ya Youssef Mehri dakika ya kwanza, Msenegal, Paul Valère Bassène dakika ya 21 na Oussama Lamlaoui, mawili dakika ya 54 na 90’+2 Uwanja wa Manispaa ya Berkane, Morocco.

DR SAMIA ATIA NENO

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hassan ameipongeza timu ya Simba kwa kuingia Fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika baada ya kuitoa Stellenbosch jioni ya leo nchini Afrika Kusini.

“Pongezi za dhati kwa Klabu ya Simba kwa ushindi katika mchezo wa Mashindano ya Kombe la Shirikisho la Soka Afrika (CAF Confederation Cup), na kuandika historia ya kufika fainali ya mashindano haya,” amesema Rais Dk. Samia .

Aidha, Mheshimiwa Rais huyo wa kwanza Mwanamke Tanzania amesema Simba imeipa heshima kubwa nchi na amewatakia kila la heri katika hatua inayofuata.

Wekundu hao wa Msimbazi wamefanikiiwa kwenda Fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika baada ya sare ya bila kufungana na wenyeji, Stellenbosch katika mchezo wa marudiano wa Nusu Fainali jioni ya leo Uwanja wa Moses Mabhida Jijini Durban

Simba wamenufaika na ushindi wa 1-0 kwenye mchezo wa kwanza wa Jumapili iliyopita Uwanja wa New Amaan Complex, Zanzibar, bao pekee la kiungo wa Muivory Coast, Jean Charles Ahoua dakika ya 45’+2.
Simba sasa inasubiri mshindi wa jumla kati ya RSB Berkane ya

Morocco na CS Constantine ya Algeria ambazo zinarudiana leo kuanzia Saa 1:00 usiku Uwanja wa Mohamed-Hamlaoui Jijini Constantine.

Ikumbukwe RSB Berkane ilishinda 4-0 kwenye mchezo wa kwanza mabao ya Youssef Mehri dakika ya kwanza, Msenegal, Paul Valère Bassène dakika ya 21 na Oussama Lamlaoui, mawili dakika ya 54 na 90’+2 Uwanja wa Manispaa ya Berkane, Morocco.

SOMA NA HII  MUONEKANO WA UKURASA WA MBELE GAZETI LA CHAMPIONI JUMAMOSI